Katibu
Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele cha
maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akipanda mti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
Katibu
Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (katikati) akiongozwa na
Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (wa pili kushoto)
kutembelea bwawa la maji na kupanda miti katika kilele cha Wiki ya Maji.
Wengine pichani kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa (kushoto) na Kaimu Mkuu
wa Idara ya Elimu Sekondari, Steven Cleophace (kulia).
Kaimu
Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (katikati) akitoa maelezo kwa
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese na viongozi kuhusu
mradi wa maji ya bwawa la Sekeididi.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed
Mlewa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji
kimkoa.
Wananchi wa kijiji cha Sekeididi Kata ya Sekebugoro wakifuatilia maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa yaliyofanyika kijijini hapo.
Baadhi
ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakielekea
katika eneo lililotengwa kwa ajili ya zoezi la upandaji miti.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameagiza wakurugenzi wa mamlaka za
Serikali za Mitaa na Maji kuhakikisha hakuna mtu anayefanya shughuli za
kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.
Telack
alitoa agizo hilo juzi wilayani hapa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba
yake na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati wa
kilele cha maadhimisho Wiki ya Maji yaliyofanyika kijiji cha Sekeididi.
Aliagiza
wakurugenzi hao kuhakikisha vyanzo hivyo vinapandwa miti ili kutunza
uoto wa asili ambao mara nyingi huathiriwa na ukame kutokana na
kukosekana kwa miti.Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao wasimamie
utekelezaji wa sheria ya utunzaji wa mazingira ili kunusuru vyanzo vya
maji, kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi
ya maji.
“Utunzaji
wa vyazo vya maji ni jambo muhimu katika upatikanaji wa maji na hivyo
ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti
eneo linalozunguka vyanzo.“Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka
2004, kifungu cha 57, kifungu kidogo cha 1 kinakataza mtu yeyote kufanya
shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji,”
alisema.
Maadhimisho
hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti kwenye bwawa la Sekeididi
ambalo litakuwa likitoa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo
hayo.Telack aliwataka wananachi kuiunga mkono Serikali katika jitihada
zake za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama katika
maeneo yao.
Alisema
miradi hiyo imeibuliwa na wananchi wenyewe kupitia vikao vyao na hivyo
wanapaswa kuendeleza jitihada zao ili kunufaika nayo kwa kuwa wasimamizi
wake.Awali akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la maji kijijini hapo,
Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya, Bernad Bwire alisema kuwa lina uwezo wa
kuhifadhi lita milioni 119.8 za maji.
Alisema
bwawa hilo linalojengwa kwa gharama ya sh. milioni 662.4 linatarajiwa
kuhudumia wananchi 16,627 wa vijiji vinne vya Bugoro, Ngwashinong’ela na
Mwagalankulu katika kata ya Sekebugoro.
Mhandishi
Bwire alisema ili kulifanya bwawa lidumu wananchi wamejipanga kuhifadhi
mazingira yanayolizunguka kwa kuzuia mifugo kuingia katika eneo la
bwawa.Aliongeza kuwa katika kipindi cha Wiki ya Maji jumla ya miti 230
imeshapandwa na kuwa wanatarajia kupanda mingine 800 zaidi katika eneo
la kuzunguka bwawa hilo.
No comments:
Post a Comment