Thursday, March 23, 2017

Qatar Yaadhimisha Miaka Kumi (10) Huduma ya Usafiri wa Anga.


Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania,Basel Haydar, akizungumza alipokutana na waandishi wa habari katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam.
Meneja muwakilishi wa Qatar nchini Tanzania Basel Haydar, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini, katika sherehe za Kutimiza miaka kumi (10) ya kutoa huduma nchini Tanzania.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa tasnia ya usafiri wa anga nchini Tanzania wakimsikiliza kwa makini meneja mahusiano ya umma (PR Manager) wa Qatar Airways Bi.Gayathri Pradeep alipokua akielezea jinsi Qatar Airways wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wateja wao.
 Wageni mbalimbali wakibadilishana mawazo walipokutana kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya miaka kumi (10) ya kutoa huduma ya usafiri wa anga wa shirika la Qatar Airways zilizofanyika Serena hoteli Dar es salaam
Wageni (waandishi wa habari) na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga wa Qatar Airways Tanzania katika picha ya pamoja katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kutoa huduma ya usafiri wa anga zilizofanyika katika Hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam. 




SHIRIKA la ndege la Qatar (Qatar Airways) limeadhimisha miaka kumi ya kutoa huduma ya usafiri wa anga kati ya miji ya Dar es Salaam na Doha huko Mashariki ya Kati jijini jana.

Sherehe hizo zilizofanyika zilihudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na wadau wa tasnia ya usafiri wa anga nchini.

Shirika hilo lilianza kutoa huduma ya usafiri huo wa anga kati ya Dar es Salaam na Doha mwaka 2007 likitumia ndege aina ya Airbus 320.

Huduma hii ilipanuka zaidi miaka mitano badaye kwa shirika hilo kuanza kurusha ndege zake moja kwa moja kutoka kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro na badaye Zanzibar mwaka 2015 ili kukidhi mahitaji ya soko lililokuwa likikua kwa kasi.

Leo hii Qatar inatoa huduma za ndege zake zinazoruka kila siku moja kwa moja kutoka Dar es Salaam, Kilimanjaro and Zanzibar kupitia Doha na kupanuka kwenye miji zaidi ya 150 huko Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Pacific na miji muhimu kama vile London, Paris, Dubai, Shanghai na Beijing.

Mtendaji Mkuu wa shirika hili Ehab Amin, alisema: Qatar Airways ina furaha kuadhimisha miaka kumi ya huduma zake hapa nchini ambazo zinalipa shirika uwezo wa kutimiza haja ya kusafirisha watalii na wafanyabiashara katika eneo hili la Afrika ambalo lina vivutio vizuri na biashara kedekede.

“Qatar Airways inajivunia ufanisi mkubwa wa huduma zake nchini Tanzania, na tunachukua nafasi hii kuwapongeza wateja wetu wanaotufanya tujivunie mafanikio haya.

Tuna heshima kubwa ya kuendelea kutoa huduma Tanzania, kujenga uhusiano na wafanya biashara kwa mtazamo wa muda mrefu na kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu kwa miaka dahali ijayo,” alisama.

Shrika limekuwa kiungo kikubwa cha watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa takriban miaka kumi yote wakitembelea vivutio vya utalii kama vile Serengeti, Selous, Ngorongoro, Zanzibar na kwingineko nchini Tanzania.

Wakati huo huo, shirika limekuwa mstari wa mbele kusaidia kukua kwa biashara katika eneo zima la Afrika Mashariki likihudumia wafanyabiashara kujitanua katika zaidi ya miji 150 duniani kote.

Ndege husafirisha abiria kila siku kutoka Uwanja wa Julius Neyrere Dar es Salaam kwenda Doha moja kwa moja kwa masaa sita. Safari huanza saa 11 na nusu jioni na kuwasili Doha saa tano na dakika 25 usiku katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamad siku hiyo hiyo. Ndege ya kurudi kutka Doha huanza saa tatu asubuhi na kuwasili Dar es Salaam saa tisa mchana.

Safari nne kati ya saba za wiki kutoka Kilimanjaro kwenda Doha hupitia Zanzibar na zilizobaki tatu kutoka Zanzibar kwenda Doha hupitia Kilimanjaro. Abiria wa Qatar Airways hujivunia huduma, takrima na ukarimu kutoka kwa wafanyakazi wake wenye bashasha na mvuto wa upendo wakitoa vyakula vitamu vilivyopikwa kwa ustadi na wapishi maridhawa na mahiri.

Abiria pia wanajivunia huduma bora ya usafiri kutoa uwanjani baada ya kushuka kwenye ndegekatika uwanja wa Hamad wenye hoteli, bwawa la kuogelea, gym, uwanja wa squash na spa.

Shirika hili linaloendelea kukua kwa kasi na huduma bora duniani linapanua huduma zake kwa kusafirisha abiria wake kwenye mjji mipya kama vile Adelaide, Auckland, Atlanta, Birmingham, Boston, Helsinki, Los Angeles na Sydney.

No comments: