Benki
ya NMB imemwakikishia Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuwa
itaendelea kutumia mifumo ya kiteknolojia ili kuwawezesha wateja wa
benki hiyo kutumia Zaidi mifumo ya kietroniki kuliko unaotumika Zaidi
kwa sasa wa malipo kwa kutumia pesa taslim.
Hayo
ya mesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker wakati wa
ufunguzi wa Kituo cha Kibiashara cha Mtwara na kueleza kuwa nia ya benki
ni kuendelea kukua Zaidi huku ikitoa suluhu ya vipau mbele vya serikali
na kujikita katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia
zakielektroniki.
“Kwa
kutumia teknolijia mbalimbali, NMB tumewekeza Zaidi kwenye kutatua
changamoto mbalimbali za wateja wetu na hivyo kutoa fursa za kutumia
Zaidi njia za benki kuliko kutumia njia za malipo kwa kutumia pesa
taslim,” alisema Ineke.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Prof. Joseph
Semboja alisema kuwa NMB imefanya maboresho makubwa na hivyo kuwa na
uwezo mkubwa wa kutoa huduma za kifedha kwa kila kada ya watanzania na
serikali kwa ujumla.
Prof.
Semboja alisema kuwaSerikali kwa sasa inamiliki hisa asilimia 32 ndani
ya benki ya NMB zenye thamani ya Zaidi ya Bilioni 430 hivyo kuiwezesha
serikali kupata gawio la Zaidi ya bilioni 75 ndani ya miaka mitano.
“Kwa
mwaka huu mheshimiwa raisi, kama mkutano mkuu wa wanahisa utakaokaa
mwezi wa sita mwaka huu, utabariki Kiwango cha gawio, serikali itapata
gawio la shilingi Bilioni 16.5 zinazotokana na faida iliyopatikana mwaka
2016,” alisema Prof. Semboja.
Nae
Rais Magufuli aliwapongeza NMB kwa huduma wanazotoa na kutoa wito kwa
viongozi wa serikali na wakuu wa wilaya na viongozi waliopo ndani ya
serikali kufanya biashara na NMB kwani serikali ina hisa kwenye benki
hiyo na hupata faida kutoka NMB.
“Nikuombe
Waziri, toa maelekezo kwa sababu wewe ndo unasimamia pesa, pesa ya
serikali ipitie NMB ili nipate gawio kubwa zaidi, wale wengine
wanaofanya biashara bila kuifaidisha serikali na kugawana gawio wao kwa
wao huku serikali haipati faida yoyote, hatutafanya biashara nao,”
alisemaRaisiMagufuli.
Rais Magufuli pia aliiomba NMB kushiriki katika kuunga mkono ajenda ya serikali katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Rais
Magufuli alisema kuwa,“Naomba NMB mshiriki katika kukopesha viwanda
hasa viwanda vidogovidogo na hivyo kuunga Mkono juhudi za serikali
katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.”
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara baada kukifungua
rasmi kituo cha Biashara cha NMB mjini Mtwara kijulikanac ho kama Mtwara
Business Centre. Pamoja na mambo mengine, rais magufuli alimuagiza
Waziri wa fedha Dr Philip Mpango kuhakikisha kuwa fedha zote za serikali
zinapita NMB.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkurgenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha kibiashara cha NMB – NMB Business Centre mjini Mtwara juzi. Kutoka kulia niAfisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati – Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi – Prof Joseph Semboja na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara – Halima Dendegu na Waziri wa Fedha na Uchumi – Dr Philip Mpango.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkurgenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha kibiashara cha NMB – NMB Business Centre mjini Mtwara juzi. Kutoka kulia niAfisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati – Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi – Prof Joseph Semboja na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara – Halima Dendegu na Waziri wa Fedha na Uchumi – Dr Philip Mpango.
No comments:
Post a Comment