Wednesday, March 15, 2017

NI WAJIBU WA MAOFISA MAWASILIANO KUHUISHA TOVUTIZAO-DKT JABIRI

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao (kulia)  akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas (kushoto) akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao.
 Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano  Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. 
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo) Bi. Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TBC Bi. Edna Rajabu akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. 
 : Afisa Habari Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambili akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
 : Afisa Habari Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambili akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia ya kidigitali kutoka  Kampuni ya Push Observer Kanali Mstaafu Dkt Abas Katalla akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani humo.

Dkt. Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni  kuhuisha matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana na wakati ili  kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

“Wakala kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.

Mtendaji Mkuu huyo ameongeza kuwa tovuti za taasisi zisitumike tu katika kutoa taarifa za huduma na bidhaa zao bali zitumike kuelezea mambo mengine muhimu yanayofanywa na taasisi hizo.

Akielezea kuhusu tovuti kuu ya Serikali, Dkt. Bakari amesema ni muhimu kuhakikisha taarifa muhimu na za kudumu za taasisi husika zinawekwa ili kusaidia wananchi kufahamu kiundani kazi wanazozifanya.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano   (TAGCO), Bw.Innocent Mungy amesema mbali na kuweka taarifa katika tovuti za Serikali, ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini kutumia mitandao ya kijamii kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi .
“Kutokana na maendeleo ya teknolojia duniani hasa katika upande wa mawasiliano, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakileta tija kwa taasisi za Umma kwani yanasaidia Serikali kujibu haraka hoja zinazowasumbua wananchi”alisema Mungy.
Pia aliwataka Maafisa Mawasiliano kuwa wabunifu katika kutumia mitandao ya kijamii kwani mitandao hiyo inatoa fursa ya kushirikiana, kutangaza huduma na bidhaa za taasisi, kufahamu matatizo ya wananchi.

No comments: