Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles
Kaijage amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za
utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na
kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.
Jaji Kaijage ameyasema hayo alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kufungua kikao
cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.
“Jukumu kubwa la Tume ni kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora
nchini, kwa maana hiyo ni muhimu kwamba watumishi wa Tume wazingatie maadili na
kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu hili” alisema na
kuongeza kuwa:
“Ni muhimu kwa watumishi wa Tume katika utendaji kazi wao kuepuka vitendo
vya ukiukwaji wa maadili kama vile rushwa, upendeleo na au ubaguzi wa aina
yoyote katika sehemu ya kazi”
Mbali na hayo, Mhe. Jaji Kaijage aliipongeza Tume kufanikisha uchaguzi
mdogo uliofanyika mwezi Januari mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za
Tanzania Bara kwa kuufanya kuwa wa amani na utulivu pamoja na changamoto
mbalimbali zilizoukabili uchaguzi huo.
Mbali na kutoa maelekezo hayo Mgeni rasmi huyo wa ufunguzi wa kikao cha
Baraza la wafanyakazi wa NEC, alitoa wito kwa wajumbe wa kikao hicho na
watumishi wote wa Tume kuitafsiri kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo na
kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali.
Alieleza matumaini yake juu ya umoja na ushirikiano uliopo Tume kwamba vitaimarika
na kuwa taasisi hiyo itatekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kujenga nguvu na
mshikamano wa pamoja kwa wafanyakazi wote.
Katika kikao hicho cha siku mbili mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo
Mapitio ya mwaka 2016/2017 na Makisio ya Bajeti ya mwaka 2017/2018, Wajibu wa
Mtumishi, Dawa za Kulevya na Athari zake kwa jamii na Namna ya Kupambana na
Ugonjwa wa Ukimwi.
“Ninaomba mjadili mada hizo kwa kina na busara mkitambua kuwa matokeo ya
majadiliano yenu ni kwa ajili ya maslahi ya Tume na taifa kwa ujumla” alisema
Mhe. Jaji Kaijage na kufafanua kuwa:
“Kwa kuwa kipind hiki ni cha bajeti nashauri na kusisitiza mjadili kwa
kina vipaumbele vya bajeti vya taasisi ili viwe ni msingi wa kuiwezesha Tume
kuwa na ubunifu na uthubutu wa kuibua mawazo mapya yatakayoiwezesha kupiga
hatua zaidi na utendaji kazi bora wa kila siku”
Aliwakumbusha wajumbe kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameundwa kwa mujibu
wa Waraka wa Rais Namba 1 wa mwaka 1970 na moja ya madhumuni ya kuanzishwa kwake
ni kuongeza ufanisi na tija kazini.
Aliongeza kuwa kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo namba 3 la
mwaka 2009, limefafanua kuwa lengo ni kutoa uwanja wazi wa majadiliano kati ya
watumihsi na waajiri katika kutoa maamuzi katika masuala ya ajira.
Hivyo aliwawaomba wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Tume watumie fursa
ya kikao hicho kuwawakilisha wafanyakazi wenzao vizuri kwani vikao vya baraza
ni sehemu muhimu ya kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kazi na kutimiza
malengo yake.
“Uzoefu unaonesha kuwa mabaraza ya wafanyakazi yanapotumika vizuri hali
ya maelewa na utulivu sehemu za kazi huongezeka na hivyo kuongeza tija kazini” alisema.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani, mbali na kuwambusha wajumbe
lengo la kuanzishwa mabaraza ya wafanyakazi, alisema baraza pia lina wajibu wa kutoa
maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha na kutekeleza malengo ya taasisi.
Aliongeza kuwa baraza pia ni eneo ambalo mwajiri anapaswa kutoa ufafanua
kwenye maeneo ambayo watumishi watahitaji kupata ufafanuzi hasa kuwasilisha
mapendekezo ya mwelekeo wa Bajeti ya Taasisi kabla haijawasilishwa kwenye
Kamati ya Bunge.
Wakati akimshukuru mgeni rasmi kwa ufunguzi, Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) Taifa Bw. Heri Mkunda alimueleza mgeni rasmi jinsi
anavyoridhishwa na jinsi baraza la wafanyakazi linavyopewa umuhimu na Tume.
Bw. Mkunda pia alimpongeza Mhe.
Jaji Kaijage kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume na kwamba Tughe Taifa wana imani naye atatimiza vyema
ujenzi wa demokrasia nchini na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwake ili
kutimiza lengo hilo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima
Ramadhani (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi wa ufunguzi
wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo Mhe. Jaji (R) Semistocles
Kaijage (kulia kwake) kabla ya kufungua kikao hicho.Kulia ni Katibu Mkuu wa (Tughe)
Taifa Bw. Heri Mkunda na kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi.
Rose Malo akiwasilisha muhtasari wa kikao kilichopita cha baraza hilo huku
Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima Ramadhani (katikati) na Naibu Katibu Msaidizi
Bi Uddy Sadiki wakifuatilia muhtasari wa kikao hicho.
Mwasilishaji kutoka Idara ya Sera
na Mipango, akiwasilisha Bajeti ya Tume kwa wajumbe wa baraza.
Mwakilishi kutoka kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti dawa za Kulevya
Tanzania Bw. Amani Msami akiwasilisha mada.
Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukiwmi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Hafidh
Ameir akiwasilisha mada.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
wakifuatili uwasilishaji wa mada.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
wakifuatili uwasilishaji wa mada.
Baadhi ya wawakilishi wa
wafanyakazi wakiulza maswali kwenye kikao.
13. Mkuu wa Idara ya
Baadhi ya wawakilishi wa
wafanyakazi wakiuliza maswali kwenye kikao.
Mjumbe wa kikao cha baraza ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango
ya Tume Bw. Silvius Nkwera akifafanua jambo wakati wa kujadili Bajeti.
Mjumbe wa kikao cha baraza ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango
ya Tume Bw. Silvius Nkwera akifafanua jambo wakati wa kujadili Bajeti.
Mgeni Rasmi wa Kikao cha Baraza
la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage
(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja ya meza kuu na wakuu wa Idara
za Tume hiyo (waliosmama).Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima
Ramadhani na Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Heri Mkunda na Kulia kwake ni Katibu wa
Baraza hilo Bi. Rose Malo na Naibu Katibu Bi. Uddy Sadick.
No comments:
Post a Comment