Monday, March 27, 2017

MTANZANIA AFUNGUA DUKA LA NGUO ZA KITANZANIA MJINI GOLDSBORO NORTH CAROLINA NCHINI MAREKANI

Mtanzania Lilian Danieli mwenye kampuni yake ya NASHONA amefungua duka la nguo za Kitanzania Goldsboro jimbo la North Carolina nchini Marekani. Uzinduzi wa duka hilo ambalo lipo Center Street katikati ya mji huo wa Goldsboro ulifanyika siku Jumamosi March 25, 2017. Anuani kamili ya duka ni 119 Center Street, Goldsboro, NC na simu ya dukani ni 918 947 1273.

Katika duka hilo nguo mbalimbali vitenge toka Tanzania ikiwa asilimia 90 ameshona yeye mwenyewe na baadhi ya vingine kuja toka Tanzania. Duka litakua linafunguliwa siku ya Jumanne mpaka Jumamosi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production
Baadhi ya wateja waliokuwepo dukani hapo siku ya uzinduzi wa duka hilo Jumamosi March 25, 2017 Goldsboro, North Carolina nchini Marekani.
Lilian Daniel Kulia akikinja moja ya nguo zilizo nunuliwa na mmoja ya wateja wake siku ya uzinduzi wa duka lake la nguo za kiTanzania lililozinduliwa siku ya Jumamosi March 25, 2017.
Kushoto ni Serena Danieli akisaidiana na dada yake Imani Danieli katika kuhakikisha mahesabu ya duka yanaenda sawa.
Lilian Danieli akiwa na mmoja ya wateja wake akiwaonyesha nguo zake na kuwapa maelekezo.
Mmoja ya wateja akilipia kitu alichonunua.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.

2 comments:

Zawadi said...

Hongera sana Lilian. Mwanzo mzuri. Umeonesha njia, wengine wafuate kwa faida yenu (diaspora) na Tanzania yetu.nakuombea mafanikio tele.

Unknown said...

Congratulations cousin Lily, this is awesome. Kila la heri!