Wednesday, March 8, 2017

MKUTANO WA KUHITIMISHA MCHAKATO WA RASIMU YA SERA YA MILIKI BUNIFU WAFANYIKA JIJINI DAR


 Kikao cha siku tano cha wabobezi/wataalamu katika mambo ya miliki bunifu,kinaendelea kufanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano katika Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Msasani jijini Dar,ambapo kikao hicho kimejumuisha Wadau kutoka Serikalini sambamba na Sekta binafsi.

Mchakato wa kikao hicho unafuatia wakati shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) lilipoanza kufanya mchakato wa tatifi ya sera ya miliki bunifu  tangu miaka minne iliyopita kwa kufadhiliwa na  wahisani ‘Best Dialogue’ ,ambapo mwaka 2013 inaelezwa kuwa tafiti hiyo ndio ilipelekwa rasmi Wizarani  kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi.

Rais wa Shirikisho la Filamu hapa nchini (TAFF),Simon Mwakifwamba,alisema kuwa Mkutano huo wa kuhitimisha rasimu ya sera ya miliki bunifu,ni sera ambayo ilipatikana kwa kufuata taratibu zote, kwa maana ya ushirikishwaji kwa upande wa serikali na Sekta binafsi,Mwakifwamba alisema kwa upande wao kama wasanii hiyo ndio sehemu yenyewe muhimu ambayo wasanii wamekuwa wakiiliia kwa muda mrefu.

"Kwa mchakato huu sisi kama wadau tunasema kwamba hapa tulipofika tuko pazuri, na nina imani na wataalamu hawa kwamba tukiwa  na juhudi za pamoja tutaweza  kuhitmisha hii rasimu hii ya miliki bunifu na mwisho  wake tutatoka na sera nzuri ,na kama tutakuwa na msingi mzuri wa kuwa na sera nzuri itatupelekea na kuwa na sheria nzuri,tukiwa na sheria nzuri tutakuwa na  kanuni nzuri,tukiwa na vitu hivyo vitatu tunaamini serikali itakuwa imetengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu wote katika nyanja   mbalimbali, kwamba hii sera itakuwa  yenye tija na mafanikio makubwa kwa nchi na hata kwetu  wasanii kwa ujumla".alisema Mwakifwamba.

 
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Biashara ya nje,Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Wilson Malosha akizungumza mbele ya wanahabari na Wadau  mbalimbali katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,Kulia ni Rais Shirikisho la Filamu hapa nchini,Simon Mwakifwamba.
 Wadau mbalimbali wakifutilia yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka meza kuu,katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadh ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,
 Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,

No comments: