Friday, March 10, 2017

MBUNGE WA KIBAHA MJINI KOKA AHIDI KULITATUA TATIZO LA MAJI KWA WAKAZI WA KATA YA PANGANI


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

WAKINAMAMA wa kata ya Pangani wanaoishi katika mitaa minne ya Lumumba,Kidimu, Liwale pamoja ma mkombozi katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kuwalazimu wakati mwingine kuamka usiku wa manane kwa ajili ya kwenda kuchota maji visimani kitu ambacho kinahatarisha usalama wa maisha yao kutokana na mazingira yenyewe kuwepo katika mapori.

Kilio hicho cha wakinamama hao wamekitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika kata ya Pangani kwa lengo ya kuweza kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuweza kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto ambazo zinawakabili.

Wakinamama hao akiwemo Maria Benjamini ,Zawadi Ibrahimu,pamoja na Asimu Mendani walisema kuwa wanashindwa kufanya shuguli nyingine za kuleta maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi wa kutafuta maji hivyo wameiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuliingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma ya maji.

Kilio cha wakinamama hao kinamgusa na kumwinua Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka na kuamua kumwagiza mbele ya mkutano wa adhara Injinia wa maji katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kuhakikisha wananchi wa mitaa minne ya Kidimu, Lumumba,miwale pamoja na mkombozi iliyopo kata ya Pnagani wanapata maji ya bomba haraka ili waweze waondokana na adha waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu.

Koka alisema kwamba suala hilo hawezi kulifumbia macho hata kidogo na atahakikisha kwamba analivalia njuga kwa lengo la kuweza kuona wananchi wake wa kata ya Pangani wanapata maji safi na salama na kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata kwa kipindi cha muda mrefu.

“Ndugu zangu wananchi wa kidimu ninachotaka kusema ni kwamba ninamwagiza Injinia wa maji kuhakikisha kwamba katika mitaa yote minne maji yanapatikana ili wananchi waweze kuondokana na usumbufu huu hususan wakinamama wanaamka nyakati za usiku kwenda kutafuta maji kitu ambacho mimi kama Mbune wenu sitaki kukiona ninachotaka ni maji,”alisema Koka.

Akijibu malalamiko yaliyotolewa na wananchi hao wa pangani Mbele ya Mbunge kuhusina na kilio chao cha siku nyingini juu ya kero sugu ya upatikanaji wa maji Injinia wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mjini Grace Limo amesema kuwa kwa sasa taratibu zote zimeshafanyika la kuweka bomba kubwa ambalo litakiuwa likisambaza maji katika maeneo mbali mbali ya Kibaha kutoka mtambo wa Ruvu juu.

KUWEPO kwa tatizo sugu la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Kibaha kusababisha baadhi ya wakinamama kuacha familia zao wakiwemo watoto watogo nyakati za usiku kwa ajili ya kwenda kuchota maji hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikali katika kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala hilo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Pangani baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwawahutubia wananchi wa kata ya pangani katika mkutano wa adhara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeeo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji wakimsikiliza Mbunge wakati akiwahutubia katika mkutano wa adhara uliofanyika katika viwanja vya mtaa wa kidimu.
Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi akifafanua jambo kwa wananchi katika mkutano huo uliondaliwa na mbunge ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).


………….

No comments: