Saturday, March 18, 2017

LAPF WATOA REFLECTOR JACKET 500 KUSAIDIA BODA BODA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI

 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya jaketi angavu (Reflector Jacket) kati ya majaketi 500 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda katika hafla iliyofanyika wilayani humo jana. LAPF imetoa majaketi hayo kwa ajili ya kusaidia waendesha bodaboda ili waweze kutambulika wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, William Gama na Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi. 
 Waendesha boda boda wa Wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Waendesha boda boda wa Wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe, akionesha moja ya jacket katika mkutano huo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya hiyo, Khamis Dikupatile.
 Waendesha bodaboda, Edward Akwilini (ukushoto) na Jackson Clavery wakijadiliana jambo kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa kuhusu mfuko huo.
 Mwendesha bodaboda,  Jackson Clavery akiuliza swali 
kwenye mkutano huo.
 Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Pikipiki za waendesha bodaboda zikiwa zimeegeshwa nje 
wakati wa mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (katikati), akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda, akijaza fomu wakati akijiunga kwa hiari na mfuko wa LAPF. Kushoto ni   Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker.


Na Dotto Mwaibale

MFUKO wa Pensheni wa LAPF umetoa jaketi angavu (Reflector Jacket) 500 kwa ajili ya kuwasaidia vijana waendesha 
bodaboda wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Happyness Seneda, katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Kisarawe jana,  Meneja Masoko na Mawasiliano wa mfuko huo, James Mlowe alisema wametoa msaada huo baada ya kuombwa na mkuu wa wilaya hiyo pia ni moja ya kazi yao ya kusaidia jamii.

"Tumetoa msaada huu baada ya kuombwa na mkuu wa wilaya lakini pia ni moja ya shughuli za jamii zinazofanywa na mfuko 
huu kwa wanachama wake" alisema Mlowe.

Kabla ya kukabidhi msaada huo Mlowe alieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo na namna ya kujiunga nao na katika hatua nyingine aliwataka waendesha bodaboda hao kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha wanazozipata katika 
shughuli hiyo ili akiba watakayoweka iweze kuwasaidia siku za usoni.

Mlowe alitumia fursa hiyo kuwaambia waendesha bodaboda hao kujiunga na mpango wa hiari wa kuweka akiba ya fedha 
zao katika mfuko huo wa LAPF ambao unamanufaa makubwa.

Mkuu wa wilaya hiyo Seneda aliwaambia bodaboda hao kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao na kuwaomba kudumisha 
hali ya usalama wilayani humo.

"Jaketi hizi mlizokabidhiwa leo hii zitasaidia kuwatambueni hivyo kuwa rahisi kumtambua mhalifu na kila mmoja wenu 
atasajiliwa kulingana na namba iliyoandikwa katika jaketi lake" alisema Seneda.

Alisema mpango wa vijana kujiunga katika vikundi imesaidia kuwezeshwa kupitia mfuko wa maendeleo wa wilaya hiyo ingawa 
alisema muitikio wa vijana wa kiume ni mdogo ukilinganisha na wanawake.

Seneda aliwataka waendesha bodaboda hao kubuni miradi mingine kama kilimo na ufugaji ili kuinua vipato vyao badala ya 

kutegemea kazi hiyo pekee.

No comments: