Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
IDADI ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa haraka kwa fedha.
Hayo
yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya
Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya
Washiriki wa Warsha ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha,
inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la Zanzibar, leo Machi 30, 2017
waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi zinachakaa haraka hususan
shilingi 500 na shilingi 1,000/_
“Ubora
wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini
matumizi makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya
idadi kubwa ya watu na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
Akifafanua
zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni
Milioni 48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio
wanatumia huduma za kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya
waliosalia, hutunza wenyewe fedha hizo.
Utunzaji
mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia
kuchakaa haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na
Kibondo mkoani Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo,
utakuta fedha inachakaa haraka sana, alisema Bw.Dollah.
Akielezea majukumu ya Kurugenzi ya Huduma
za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria
namba Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa,
kusambaza na kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.
Pia
Kurugenzi hii ina jukumu la kutoa huduma za kibenki kwa serikali zote
mbili, (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar).
Alisema jukumu lingine kubwa la Kurugenzi hiyo ni kuhakikisha
uwepo wa noti na sarafu kwa uwiano wa kutosha kwenye uchumi, “hatuwezi
kuingiza fedha nyingi kwenye uchumi bila ya kuangalia uwiano wa
uzalishaji na kiwango cha fedha”.aliongeza.
Akizungumzia
kushuka na kupanda kwa thamani ya fedha ya Tanzania, (TZS), Mchumi
Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa
BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, alisema, miongoni mwa sababu zinazopelekea
hali hiyo ni uhitaji wa fedha yetu, (TZS), katika soko(mzunguko).
“Ili
fedha yetu (TZS), iwe na thamani lazima uhitaji wake uwe mkubwa katika
soko, na ikitokea kwamba fedha yetu inahitajika kwa wingi basi fedha
yetu itapanda thamani na hii itatokana na kuongeza uzalishaji na kuuza
bidhaa zetu nje, lakini endapo uzalishaji utapungua, na Nchi ikaingiza
kwa wingi bidhaa kutoka nje, itapelekea uhitaji wa Shilingi kupungua na
hivyo thamani yake pia itapungua.” Alisema Lusajo. Na kushauri taifa
kama taifa liongeze thamani ya bidhaa ili ziweze kuuzwa nje na hivyo
kuongeza uhitaji wa fedha yetu.
Aidha,
BoT, imesema, utafiti mdogo iliyofanya umeonyesha kuwa wateja wengi
katika benki za biashara, wanapokwenda kuchukua fedha, hupokea fedha
(noti), za thamani ya juu yaani 10,000, na 5,000 licha ya kuwa wengine
wangependa kupewa fedha ndogo ndogo kwa ajili ya urahisi wa kupata
chenji.
“Ni
haki ya mteja wa benki za biashara anapokwenda kuchukua fedha benki,
kudai apewe fedha za chenji (fedha ndogo ndogo, yaani 500/- 1,000,000/
na 2,000/=, ili kumrahisishia anapokwenda kufanya manunuzi asipate shida
ya chenji.” Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi
Vicky Msina alibainisha.
Washiriki wa semina, wakiangalia noti ya Sh. 10,000, ili kutambua kama ni halali au so halali.
Maafisa wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, (kulia), na Bw. Mohammed na Mohammed Kailwa, wakijadiliana jambo kwenye komppyuta
Baadhi ya maafisa kutoka BoT
Mtangazaji wa Channel Ten, Bi. Dorcas R. Mtenga, akizungumza
|
Bw. Dollah akitoa mada
Mchumi
Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa
BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akitoa ufafanuazi kuhusu kwa nini thamani ya
shilingi ya Tanzania inapanda na kushuka
Bw. Dollah(kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, Bw. Lwaga Mwambande
Maafisa wa BoT
No comments:
Post a Comment