Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo
ya muda mfupi, ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY iimeendesha mafunzo ya
juma moja ya Itifaki na Uhusiano wa Kibiashara ‘PROTOCOL AND BUSINESS ETIQUETTE SHORTCOURSE kati ya tarehe 22 -25 February, 2017. Mafunzo haya yalilenga
kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi.
Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya
muda mfupi yatolewayo na ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY kila mwezi,
katika mafunzo hayo
ambayo Kwa kawaida wawezeshaji
wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea
katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya
kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao.
Mafunzo hayo ya wiki moja
yaliyofanyika Dar es salaam (katika ukumbi wa mikutano wa Dar es Salaam Convention Centre -
DCC), washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe
za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali pamoja na kuandaa mikutano ya
kibiashara, tabia njema za kibiashara, kanuni za Mavazi na kupokea wageni
mashuhuri na kuwahudumia. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na
namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma, yalihusisha
maofisa 24 wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali , vyuo vikuu na sekta
binafsi pamoja na maafisa kutoka katika Balozi zinazowakilisha nchi zao
Tazania.
(Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni Ndugu Lucas Jackson)
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi
wa Mafunzo na Operesheni wa ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY Ndugu Lucas
Jackson alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha
utendaji wa kazi zao na kuleta ufanisi mahala pa kazi hivyo kuna haja ya
waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kupata mafunzo kama haya na mengine
yatolewayo na EONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY ili kuwajengea uwezo
watanzania hasa katika Diplomasia ya Uchumi na uchumi wa viwanda Tanzania, na
hivyo kuzalisha wataalam wenye weredi wa uchumi wa viwanda na Diplomasia ya
Uchumi.
Akizumgumzia mafunzo yaliyohitimishwa ya Protocol and Business Etiquette; alisema
“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa kibiashara (Protocol and Business Etiquette) zinahitaji utaalam ambao utamfanya
mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo
mazuri. Hivyo mafunzo haya ya kivitendo ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa
na ECONOMIC DIPLOMACY
–TRAINING ACADEMY yana lengo la
kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi
na kupata matokeo bora,”
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni Ndugu Lucas
Jackson,
akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY
itaendesha mafunzo ya wiki moja ya UTATUZI WA MIGOGORO NA USULUHISHI (CONFLICT RESOLUTION) mnamo tarehe
22 -25 March 2017 yatakayofuatiwa naya
DIPLOMASIA YA UCHUMI ; Biashara na uwekezaji (ECONOMIC DIPLOMACY: Trade and
Investment Promotion) mnamo tarehe 5 – 8April, 2017 hapa DCC –Dar es salaam,
na kuwataka wale wote wanaohitaji kupiga
namba 0713667303 au lucassoona@yahoo.com kwa maelezo
zaidi na kupewa utaratibu.
AU kuwasiliana moja kwa moja na:
Kurugenzi ya Mafunzo na
Operesheni,
Economic diplomacy –Training Academy
Mob: 0763657587
Website: www.economicdiplomacy.ac.tz/training
www.economicdiplomacy.ac.tz
No comments:
Post a Comment