Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya CRDB imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kufungua akaunti ya Malkia ambayo itakuwa ni yenye malengo yakinifu na manufaa kwa maendeleo kwa wanawake.
Akizungumza na Globu hii, Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura amesema kuwa akaunti hii ya Malkia inakuwa na malengo makuu ya kumuwezesha mwanamke ili aweze kuwa na malengo yakinifu ya kujiendeleza kiuchumi.
Mary amesema kuwa, kampeni hii imeanza machi mosi na itakuwa ni endelevu na taratibu zake za kufungua ni kwa kima cha chini cha shilingi cha elfu hamsini (50,000) na mteja atatakiwa kuweka hela kwa muda wa mwaka mmoja bila kuzitoa.
Amefafanua kuwa, ndani ya mwaka mmoja mteja anaweza kupata faida ya kutosha na kuanzisha miradi mbalimbali.
Mkurugenzi wa tawi la CRDB Water Front Donath Shirima (kulia) akiwa pamoja katika picha na wafanyakazi wa tawi hilo kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani Machi 08 mwaka huu.
Wafanyakazi wa wa tawi la CRDB Water Front katika picha za pamoja kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani Machi 08 mwaka huu.
Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura akiwa anatoa maelezo ya namna ya kufungua akaunti ya Malkia kwa wanawake inayolenga kumnufaisha mwanamke.
Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma katika moja ya madirisha ya benki hiyo tawi la Water Front.Picha Zote na Zainab Nyamka.
No comments:
Post a Comment