Thursday, March 16, 2017

CHAMA CHA MADAKTARI WA AFYA YA KINYWA NA MENO KUFANYIA MATIBABU WATOTO 53

Daktariwa Kinywa na Meno Hospitali ya Sinza Dar es Salaam, Idd Khery akimfanyia matibabu ya Kinywa na Meno mwanafunzi wa Darasa la 3 Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija, Rajabu Yahaya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo kuelekea Wiki ya Kinywa na Meno ambapo watoto 53 jana na leo wamepatiwa huduma hiyo bila malipo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya (wa pili kulia) akifunga Wiki ya Kinywa na Meno Mkoani humo katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga leo, kuanzia kushoto ni Dkt. Anold Gemoniani kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Mwalimu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Profesa Bakari Lembariti ,Daktari Bingwa wa Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro (wa pili kushoto) akimtambulisha Dkt, Arnold Mtenga wakwanza kushoto kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi (kulia) mara alipoongozana na ujumbe wake kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza matibabu katika Kituo cha watoto Buhangija, wa tatu kushoto ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi (kushoto) ambapo kaimu Mkurugenzi huyo alisema, napenda kuwashukuru katika kuja kusaidia kutowa huduma hiyo kwa miaka 3 mfululizo na akasema, nawaomba kujipanga tena kurudi ili kutowa elimu kwa wakubua na ninaona kwa sasa kunamaboresho makubwa yamefanyikakwa watoto wetu na lengo hasa ni kusiwe na matatizo ya meno kwa watoto hao nawaomba mjekila mwaka natutazidi kuwapa ushirikiano kwani watoto hao niwakwetu sote, kama mnavyojuwa Serikali inawadau tutashirikia nao na kama kunapahala tulikosea mtusamehe na mwisho niisiwachoshe sana niwatakie safari njema ya kuelekea Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi katika picha ya pamoja na madaktari.

Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro akizungumza na walimu wa Shule ya Jumuishi Buhangija (pichani hawapo) aliwashukuru kwa mapokezi yao na kutowa wito kwa walimu kuzidi kuwa karibu na watoto hao kwani niwatoto wetu na pamoja na mafanikio makubwa ya elimu ya upigaji mswaki kwa watoto hao niwakati wa kuzidi kuwanao karibu, alisema, Carneiro , tunaondoka Buhangija tukiwa tumeona mabadiliko makubwa ya mwaka wa kwanza , wapili na watatu tukiwa na furaha ya watoto kutambua umuhimu wa kutunza kinywa na meno yao, mwisho nawatakia kila la heri katika kusaidiana kuwalea watoto hao kwa kushirikiana kwa pamoja.
Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya akizungumza na mwanafunzi wa Shule ya Awali ya Buhangija Mkoani Shnyanga, Mck Machia kushoto na kulia ni mwanafunzi wa shule hiyo, Pasi Mugisi.

No comments: