Wednesday, March 15, 2017

Ajali: Lori lililobeba mawe yaua Mtu Mmoja Makete

Na Edwin Moshi wa Eddy Blog
Lori lililokuwa limebeba mawe limepinduka katika kijiji cha Masisiwe wilayani Makete na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika lori hilo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo limepoteza muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani. Ajali hiyo inadaiwa kutokea kati ya saa nane na saa tisa alasiri hii leo.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema Lori hilo lilikuwa linatoka kubeba mawe kwa ajili ya kujenga daraja katika kata ya Ipepo kabla ya kupoteza mwelekeo likiwa njiani na kupinduka kisha kuporomokea bondeni.
Jeshi la polisi Makete limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi. Tutawaletea taarifa kamili ya tukio hilo pindi mamlaka husika zitakapatia.

Polisi wakipima jinsi ajali hiyo ilivyotokea 
 Askari Polisi akiangalia mawe yaliyokuwa yamebebwa na lori hilo kabla ya kutokea ajali





Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi
Lori hilo likionekana kwa mbali baada ya ajali


Muonekano wa lori hilo baada ya ajali




Ajali ilipoanzia, hapa ndipo lori hilo lilipotumbukia 

No comments: