Tuesday, February 7, 2017

WAZIRI LUKUVI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA TANGA NA MANYARA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza  kwenye kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya kuumaliza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Dokta Joel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala 
Baadhi ya wenyeviti wa halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo
WAZIRI wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William  Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.

Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi
  kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake  mkoani hapa.

Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi
  ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

"Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya kazi
  hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji"Alisema Lukuvi.

Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo
  mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa  mara ya tatu na litakuwa la mwisho.

Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji
 
kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale
panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya kuuwongeza.

"Kama kuna viongozi wanamatakwa yao basi watambue hawatapata nafasi na
  tayari tulishapokea agizo kutoka Waziri Mkuu na kinachotakiwa hapa ni utekelezaji wa kumaliza mgogoro huo"Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela alisema jukumu kubwa
  lililopo mbele yao ni kutoa ushirikiano kwa timu iliyoundwa na Wizara hiyo na kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa wakati kama Waziri alivyoagiza.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera alisema lazima viongozi
  washirikiane kwa pamoja kutatua mgogoro huo ambao umekuwa ni tatizo kwa Wilaya hizo mbili na kupongeza hatua ya Serikali ya uhakiki upya hasa kwa kufuata GN ya namba 65 ya mwaka 1961 kama alivyoagiza Waziri Mkuu na si vinginevyo.

Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya
  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.

Majaliwa alisema katika ziara yake hiyo kuwa Aidha alisema baadhi ya
  viongozi wa kisiasa na Serikali kwa kutokuwa wa kweli mbele ya wananchi kuhusiana na mgogoro huo na wanajaribu kufanya maamuzi kwa ajili ya maslahi yao ya kujiaminisha mbele ya wananchi hao.

Alisema lazima ramani ya mwaka 1961 ifuatwe na viongozi waache kuwa na
  agenda zao za siri na kuwadanganya wananchi kwa kuanza kurudia kupima mpaka huo mara kwa mara bila ya kupata majibu sahihi ramani na huu ni muda wa kuwael3za ukweli wananchi

"Ramani ipo ya mwaka 1961 na najiuliza sana hivi hao wanaokuwa na
  tabia ya kurudia kupima pima mara mbili agenda yao ni nini,huu si udanganyifu kwa wananchi?"Alihoji Majaliwa.

Alisema kuananzia sasa GN itakayotumika ni ile namba 65 ya mwaka
  1961,zaidi wanachotakiwa wataalamu kukifanya ni kuimarisha mpaka huo kwa kuwashirikisha  viongozi wa Serikali,wanasiasa na wananchi ili kuweka mustakabali mzuri juu ya mpaka huo
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog

No comments: