Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
(kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa
kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia
sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na msambazaji wa filamu nchini Bibi. Rose Urio akichangia mada
wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza
akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu
kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea
kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
(wanne kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya filamu
walioshiriki katika kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es
Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia Wambura, watano kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole
Gabriel na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
Picha na: Genofeva Matemu WHUSM.
No comments:
Post a Comment