Monday, February 6, 2017

Vyama vya Siasa Vyatakiwa Kutoa Fursa za Uongozi kwa Wanawake

Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akiwasilisha mada katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akifafanua jambo katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo Sehemu ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakifuatilia mada anuai. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo.

 BAADHI ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya Tatu za Mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wameviomba vyama vya siasa kutoa fursa za uongozi kwa wanawake ili waongezeke katika nafasi za uongozi ngazi mbalimbali. 

Ombi hilo limetolewa na viongozi hao katika maoni yao walipokuwa katika semina kuangalia usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). 

Baadhi ya viongozi hao na watendaji walisema kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya vyama vya siasa ambazo zinaendelea kuwa vikwazo kwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongoni katika vyama anuai, hivyo kama zikiangaliwa zinaweza ongeza hamasa kwa wanawake kupata nafasi za uongozi. Semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni ikiendelea.[/caption]   [caption id="attachment_77379" align="alignnone" width="800"] Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.

 Hata hivyo wamewataka wanawake kuendelea kujitokeza, kujiunga na vyama mbalimbali vya siasa pia kushiriki kugombea nafasi ili waweze kuonekana na kukwaa nafasi hizo. "Mbali na Vyama vya siasa kutakiwa kuregeza masharti na kutoa fursa kwa kundi la wanawake, wao pia wanatakiwa kujitokeza kushiriki katika siasa...na hata kugombea nafasi mbalimbali ili waonekane," alisema mmoja wa washiriki wa semina hiyo. 

Kwa pamoja viongozi hao walikubaliana kuendelea kuwaunga mkono kundi hilo katika ushiriki wa siasa ili kujenga usawa wa kijinsia katika nafasi za maamuzi kuanzia ngazi za chini na kuendelea. Kwa upande wake Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba akiwasilisha mada katika semina hiyo alisema wanawake ni wadau muhimu katika shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu ya kupewa nafasi ili waingie katika vyombo vya maamuzi. 

Alisema yapo matamko mbalimbali ya juu ya umuhimu wa kundi hilo kushiriki katika uchaguzi, japokuwa utekelezaji wake kivitendo umekuwa na changamoto kadhaa. Aidha alitolea mfano matamko hayo ni pamoja na Tamko la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (U 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW: 1979) na mpango kazi wa Beijing (1995). 

Pamoja na hayo alisema licha ya kundi hilo kusahaulika lakini limekuwa likitumiwa na vyama vya siasa kuhamasisha na kueneza sera zao ikiwemo kuongeza wanachama jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa umuhimu hivyo kupewa fursa katika ushiriki.  

No comments: