Monday, February 20, 2017

TEA YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU NA KAMPUNI YA SUNSHINE

MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku akibainisha kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya Sunshine.

“Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.

Akiishukuru TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Alisema kampuni yake imeingia Tanzania mwaka 2012 na tayari imetumia zaidi ya Dola 500,000 za Marekani katika elimu kwa miaka mitano ya uwepo wao hapa Tanzania.

“Tumedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha mazingira ya upatikanaji wa elimu yanakuwa rafiki na yenye kuvutia. Tunaamini TEA watatusaidia kuzifikia shule zenye uhitaji zaidi ili watoto wetu wapate elimu bora kwa ajili ya kujenga taifa imara,” alisema Sun.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima akifafanua jambo wakati  wa hafla ya kutiliana saini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
 Mkutano ukiendelea.

Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.
Picha ya pamoja.

No comments: