Tuesday, February 7, 2017

SIMUTV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dkt John Magufuli ametoa agizo kwa majeshi yote nchini kushiriki katika vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa kuwakamata wote wanaohusika; https://youtu.be/Uxb-bF82jUI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda ametoa siku kumi kwa viongozi wa mitaa na wazazi kuwafichua wale wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya; https://youtu.be/jy8csQ5eSOA

SIMU.TV: Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari mkoani Kilimanjaro imefikia nane baada ya majeruhi aliyelazwa KCMC kufariki; https://youtu.be/5h2XLA-Fjno

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu yupo mjini Dubai kushiriki katika mkutano wa jumuiya ya wanawake wa Falme za Kiarabu; https://youtu.be/p15ZJpPYiBc

SIMU.TV: Waziri wa Habari Nape Nnauye ameliomba bunge kutenga fedha za kutosha ili kuliwezesha shirika la habari TBC kutenda kazi kwa ufanisi zaidi; https://youtu.be/H3JYkOI-edo

SIMU.TV: Katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi amesema serikali imeanza kutoa ajira baada ya kujiridhisha kukamilika kwa watumishi hewa; https://youtu.be/lCGZAtkBiPg

SIMU.TV: Waziri wa Ardhi William Lukuvi amekutana na viongozi wa mkoa wa Tanga na Manyara ili kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya mikoa hiyo miwili; https://youtu.be/36O9lfBkoIc

SIMU.TV: Rais Dkt John Magufuli amewataka mabalozi wa watanzania kuhakikisha wanaitangaza nchi yao na kuwashawishi wawekezaji kuja nchini; https://youtu.be/m2-I5Hl71_E

SIMU.TV: Bodi ya ununuzi Tanzania inawataka maafisa ugavi nchini kuwa waadilifu katika utendaji wa kazi zao kwa lengo la kuleta maendeleo nchini; https://youtu.be/uI0msXRu1Hc

SIMU.TV: Maonyesho ya wajasiriamali yanataraja kufanyika mkoani Dodoma kwa lengo kuonyesha teknolojia zinazotumika kwenye viwanda vidogo vidogo; https://youtu.be/w8nqAouQEdU

SIMU.TV: Fahamu jinsi mauzo ya hisa yalivyopanda na kushuka katika soko kuu la hisa la jijini Dar Es salaam DSE; https://youtu.be/GnpaJD0EJ1I  

SIMU.TV: Mashabiki wa soka nchini Tanzania wameelezea mtazamo wao juu ya kitendo cha timu ya taifa ya Cameroon kunyakua ubingwa wa AFCON; https://youtu.be/cwF3JNEfz5g

SIMU.TV: Serikali imeipongeza timu ya Serengeti Boys kwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya AFCON kwa vijana mwezi April nchini Gabon; https://youtu.be/vfodF162fUA

SIMU.TV: Kamati ya saa 72 ya ligi kuu Tanzania bara imemfungia kocha wa Stand United Hemed Moroko kwa kosa la utovu wa nidhamu; https://youtu.be/bqrl_eqmsVo

No comments: