Sunday, February 5, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Jeshi la polisi limewasimamisha kazi askari kumi na wawili waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo. https://youtu.be/ldb8SxmpXP0

SIMU.TV: Wakulima wa zao la korosho wilayani Mkinga mkoani Tanga wameeleza kunufaika na minada ya kuuza zao la korosho tofauti na zamani walipokuwa wakiuza kwa mfumo wa kangomba. https://youtu.be/irJ39gzuPn0

SIMU.TV: Chama cha waalimu mkoani Rukwa kimewaaga walimu 18 walio staafu kazi na kuwapatia mabati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6. https://youtu.be/yv5YRGj3qRA

SIMU.TV: Watanzania wametakiwa kuondokana na utamaduni uliojengeka wa kujiweka mbali na shughuli za mahakama jambo linalopelekea kupoteza haki zao za msingi. https://youtu.be/2XtQZmYSzds

SIMU.TV: Ukosefu wa miundo mbinu ya maji na uchakavu wa barabara katika jengo la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Songea umeelezwa kuathiri utendaji wa watumishi. https://youtu.be/UfhdtkZLAHw

SIMU.TV: Maelfu ya wapenda soka katika mji wa Songea mkoani Ruvuma jana walishuhudia mtanange kati ya Simba na Majimaji ambapo Simba iliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa bila. https://youtu.be/wo1lbH7Vngg

SIMU.TV: Timu ya vijana ya mpira wa wavu ya Jeshi Stars wanawake na Polisi Marine wanaume wameibuka na ushindi katika michezo ya ligi ya vijana ya mpira wa wavu. https://youtu.be/LxfXUqNfG_8

SIMU.TV: Mwanasheria mkuu wa Serikali George Masaju amewashauri wabunge kuzingatia sheria na kanuni za bunge wanapochangia hoja zao; https://youtu.be/DOwpsp3smR8

SIMU.TV: Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu, ametoa wito kwa vijana wa CCM kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali ndani ya chama; https://youtu.be/SlTHM7mUAU8

SIMU.TV: Umoja wa wafanyabiashara wadogo mkoani Mwanza wamesema hawakubaliana na uamuzi wa kuunda umoja wa Machinga wilaya bila kushirikisha ule wa mkoa; https://youtu.be/8z3EmbkbJjM

SIMU.TV: Watu zaidi ya 300 waliojitokeza kupima macho katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar Es salaam wamegunduliwa kuwa na matatizo ya macho; https://youtu.be/XOqtjhM_uwg

SIMU.TV: Mwenyekiti wa jumuiya ya watu wenye magonjwa yasiyoambukiza Dr Msafiri Majirani ametoa wito kwa serikali kuanzisha mfuko wa kutibu watu wenye maradhi ya Saratani; https://youtu.be/RcjLp_1TkFs

SIMU.TV: Goli la pekee la Alain Traore lilitosha kuipatia ushindi Burkina Faso na kutwaa medali ya shaba katika michuano ya AFCON ambapo Fainali yake itapigwa hapo baadae; https://youtu.be/sM1uw5O6Mxw

SIMU.TV: Timu ya Simba imefufua matumaini ya kunyakua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara baada ya hapo kuibamiza Majimaji ya Songea kwa mabao 3-0; https://youtu.be/sqeKgEa6JAE

No comments: