Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa,
utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu (REA)utakuja na umeme mwingi kutokana na kujengwa kwa njia za
kusafirisha umeme wenye msongo mkubwa.
Profesa Muhongo aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya
kukagua utekelezaji wa REA Awamu ya Pili , katika Wilaya za Rorya na
Butiama mkoa wa Mara ambapo pia alieleza mipango ya Serikali katika
utekelezaji wa REA awamu ya Tatu.
Prof. Muhongo aliongeza kuwa, REA III itajikita katika kuyafikia maeneo
yaliyorukwa katika awamu ya I na ya pili, kuyafikia maeneo ambayo
hayajafikiwa kabisa na nishati hiyo, vilevile awamu hiyo itajikita katika
matumizi ya nishati jadidifu hususan katika maeneo yote ya visiwani.
Vilevile, alisema kuwa, lengo la Serikali kupeleka umeme mwingi na wa
uhakika katika maeneo ya vijiji ni kuchochea mapinduzi ya viwanda vidogo
vidogo na hivyo kuwataka wananchi kuachana na siasa badala yake
wajikite katika shughuli za kiuchumi ili kuchochea maendeleo ya kijamii na
Taifa kwa ujumla.
" Wananchi tunatakiwa kuachana na siasa badala yake tujikite katika
shughuli za kiuchumi. Tuzungumzie uchumi na maendeleo. Umeme ndio
kichocheo kikuu cha uchumi na ndiyo maana Serikali inatekeleza mradi wa
REA ili kufikia azma hiyo," amesisitiza Prof. Muhongo.
Pia, Prof. Muhongo alisisitiza suala la fidia katika utekelezaji wa REA
awamu ya tatu na kueleza kuwa, serikali haitatoa fidia kwa wananchi
watakaotoa maeneo yao ili kupitisha nguzo za umeme na kueleza kuwa,
wanaotaka fidia wachague kati ya fidia au kupelekewa nishati hiyo.
REa Awamu ya Tatu inatarajia kutekelezwa kuanzia mwezi Machi
mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Mhandisi Hamis Komba alimweleza Profesa Muhongo kuwa,
Shirika hilo limeridhia kutoa sehemu ya eneo lake katika mgodi wa
Buhemba linalotumiwa na wachimbaji wadogo ili waweze kulitumia kwa
shughuli za uchimbaji madini .
Mhandisi Komba amesema kuwa, eneo hilo linaendelea kupimwa ili kujua
ukubwa wake na kuongeza kuwa shughuli ya kuligawa kwa vikundi 13
vilivyojiandikisha litafanywa siku ya jumatatu tarehe 27 Februari, 2017,
baada ya ukubwa wa eneo husika kujulikana.
Kutokana na kutoa eneo hilo ambalo lilikuwa linamilikiwa na STAMICO,
Mhandisi Komba amewataka wachimbaji watakaopewa eneo husika
kufanya shughuli za uchimbaji unaozingatia usalama, Sheria na taratibu za
uchimbaji madini.
Profesa Muhongo alitembelea Wilaya za Rorya na Butiama katika Kata za
Mirwa, Tai na Muriaza tarehe 23 Februari,2017
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiongea
jambo wakati akiwaeleza wananchi na wanafunzi wa Shule ya Msingi na
Sekondari ya Nyamagongo Wilaya ya Rorya kuhusu utekelezaji wa Mradi
wa REA Awamu ya III. Shule hiyo ni miongoni mwa maeneo ambayo
yatafikiwa katika mradi wa REA awamu ya Tatu. Wengine wanaofuatilia ni
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga,
(katikati) Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rorya, Sospeter Kswahili (wa
kwanza kulia). Wengine ni Mtaalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini
Mhandisi Emmanuel Yesaya na Mkandarasi wa Kampuni ya Angelica
International.
Afisa Uhusiano na Huduma za Jamii kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), James Vesso, akitoa elimu kuhusu Kifaa cha
Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha Muriaza Kata ya
Muriaza Wilaya ya Butiama wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na
Madini kijijini hapo. Kifaa hicho hakihitaji mtandao wa umeme katika
nyumba.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos Maganga,
akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini
wananchi wa Nyamagongo ambapo Waziri na wataalam wa REA na
TANESCO wameeleza kuhusu utekelezaji wa REa Awamu ya Pili na ya
Tatu. Wengine ni Mameneja wa TANESCO, Wilaya ya Rorya na Mkoa wa
Mara, na Wataalam kutoka REA na TANESCO.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha na viongozi wa Mkoa,
wakimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(kulia) wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kukagua miradi ya REA awamu
ya II na kueleza mipango ya Serikali kuhusu utekelezaji wa REA Awamu ya
Tatu.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi
Hamis Komba, akiwaeleza wachimbaji wadogo kuhusu shirika hilo kuridhia
kutoa sehemu ya eneo lake la Buhemba kwa ajili ya wachimbaji kufanya
shughuli za uchimbaji madini.
Mtendaji Kata wa Mirwa, Neema Philipo,akisoma majina ya vikundi vya
wachimbaji wadogo ambavyo vitapewa sehemu ya eneo la STAMICO,
Buhemba. Wengine wanaofuatilia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (wa pili kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa STAMICO,
Mhandisi Hamis Komba, (wa kwanza kushoto) Kamishna Msaidizi wa
Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mhandisi Juma Sementa na
Watendaji kutoka STAMICO na wachimbaji wadogo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoa rambirambi
kwa baadhi ya wazazi ambao mmoja wa wachimbaji wadogo alifariki katika
ajali ya kifusi iliyotokea katika mgodi eneo la Buhemba, Mkoani Mara.
Sehemu ya wananchi wa wananfunzi katika eneo la Nyamagongo Wilaya
ya Rorya Mkoa wa Mara wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo, hayupo pichani.
Naibu Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Jackton Manyerere (wa pili kulia)
akiongea jambo wakati Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo (katikati) akitoa heshima katika Kaburi la Baba Mzazi wa
Manyerere., Jakcton Nyambereka Nyerere aliyefariki dunia tarehe
19/2/2017/. Wa kwanza kulia ni Mhariri wa gazeti la Mtanzania Kulwa
Keredia. Kushoto ni baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari. Waziri alifika kuhani msiba wa wahariri hao Manyerere na Keredia
wakati wa ziara yake Wilayani Butiama.
No comments:
Post a Comment