Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza amewaonya watumishi wa serikali ambao wanakwepa kushiriki mazoezi ya pamoja katika uwanja wa Samora na kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki kubanwa.
Alisema pamoja na kuwa mazoezi hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja kujikinga na maradhi yanayosababishwa na kutofanya mazoezi ila bado mazoezi hiyo ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais kwa kila mtanzania.
Hivyo alisema kutokana na baadhi ya watumishi hasa wanawake kukwepa mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana watumishi wote wanaokwepa mazoezi kwa kuitisha mazoezi siku ya kazi ili wale ambao watashindwa kufika watawajibishwa .
"Naangalia ni siku gani ambayo itakuwa ni siku ya kazi kama ijumaa ama siku nyingine yeyote ambayo nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi yangu hadi Samora kwa kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini watumishi wakichelewa ni sawa lengo kuweza kufanya mazoezi na kutekeleza agizo la serikali ......nashangazwa sana awali wanawake ndio ambao walikuwa wakifika kwa wingi mazoezini ila leo hii idadi ya wanawake imepungua ukilinganisha na wanaume ....nawashangaa sana wanawake wanaokwepa mazoezi wakati ndio ambao wanakula vitu vyenye mafuta "
Hivyo alisema kuanza sasa kila mtumishi wa serikali lazima kufika katika mazoezi na utawekwa utaratibu wa kuorodhesha majina kila idara ya watu wanaoshiriki mazoezi .
|
No comments:
Post a Comment