Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, Leo february 22,2017 ameendelea na ziara yake ya kikazi kwa siku ya tatu katika Wilaya ya Monduli ambapo yupo wilayani humo kwa ziara ya siku tano ambapo ijumaa ya wiki hii atakamilisha ziara hiyo.
Akiwa kwenye ziara hiyo leo ametembelea Zahanati ya Mswakini Juu iliyopo Wilayani humo na kujionea utendaji kazi,na maendeleo ya zahanati hiyo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi waishio jirani na kituo hicho cha Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiwasili kwenye Zahanati ya Mswakini Juu Wilayani Monduli.
kutoka kushoto Mkuu wa mkoa akikagua maendeleo ya zahanati,Aliyeshika fimbo ni Mbunge wa Monduli Julius Kalanga,kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) akiwa ameambatana na wajumbe wake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Akigagua baadhi ya mashine katika kwenye zahanati hiyo.
Mkuu wa Mkoa Akisalimiana na wananchi wa Mswakini juu waliohudhuria kwenye ziara hiyo.
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga Akihutubia wananchi wa Mswakini juu.
Mkuu wa Mkoa Akikagua baadhi ya nyumba za wauguzi wa Zahanati hiyo ya Mswakini juu. Picha na Msumbanews blog
No comments:
Post a Comment