Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Ushirika wa Vikundi vya Biashara Dar es Salaam (Vibidar Namaingo), Grace Lobulu katika sherehe iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo, Ubwa Ibrahim. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Na Richard Mwaikenda
SERIKALI imeutaka Ushirika wa Vibidar Namaingo kuanza kuzalisha mazao mengi kwa ajili ya malighafi ya viwanda vilivyopo na vinavyotarajiwa kuanzishwa nchini.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo wakati wa sherehe ya kukabidhi cheti kwa ushirika huo wa Vikundi vya Biashara Dar es Salaam (Vibidar), kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga.
Mashingo, aliipongeza Kampuni ya Namaingo Business Agency Ltd, kwa kuanzisha vikundi hivyo vya ujasiriamali na kuviatamia hadi kufikia kuunda ushirika wa Vibidar utakaoongeza viwango vya maarifa, taaluma pamoja na tija, jabo litakalowezesha wajasiramali wengi kuondokana na ujasriamali mdogo kwenda kwenye ujasiriamali mkubwa na hatimaye kuongeza pato la kaya na Taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa ushirika huu umekuja wakati muafaka, wakati Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikitoa kipaumbele katika kuhamasisha maendeleo ya sekta ya viwanda, ambapo sekta ya kilimo kupitia vikundi shirikishi inayo fursa kubwa ya kuweza kuzalisha malighafikwa ajili ya maendeleo ya viwanda.
"Ushirika wa vikundi mbalimbali kama Vibidar, vina uwezo wa kuzalisha malighafi ya kutosha kwa ajili ya kusindika mazao kutosheleza mahitaji ya viwanda, hivyo ushirika huu umeanzishwa katika muda muafaka wakati serikali inatilia mkazo katika kuchochea maendeleo ya sekta za kiuchumi zinazoweza kuchoche viwanda nchini," alisema Mashingo.
Mashingo, aliahidi serikali kuendelea kushirikiana na wadau kuimarisha ushirika ili kuzitatua changamoto mbalimbali kwa kutumia mikakati na mbinu za kila aina. Alizija baadhi ya changamoto zinaikabili sekta ya kilimo kuwa ni;uongezaji wa tija katika uzalishaji, mifumo ya soko yenye mpangilio mzuri, kujenga mitandao thabiti ya mawasiliano na kuwaunganisha wadau katika mlolongo wa thamani.
Hakusita kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Vibidar, Ubwa Ibrahim kwa bidii ya kuanzisha ushirika huo kwa Dar es Salaam tayari una vikundi 60 vyenye wanachama 4,000 waliotimiza vigezo, pia kwa kuanzisha Vikundi vya Biashara Vijijini (VIBIVI) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Ruvuma, Njombe, Tabora, Manyara, Kagera, Tanga, Kigoma, Mbeya, Songwe, Morogoro na Dodoma.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Mashingo, Mkurugenzi wa Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim, alisema kuwa kampuni hiyo kupitia Vibidar na Vibivi hutoa mafunzo kwa wajasiriamali ya jinsi ya kuendesha kilimo biashara na ufugaji wenye tija na kwamba hivi karibuni tayari wamezindua mradi wa ufugaji sungura wa kopa sungura lipa sungura katika eneo la Majohe, Dar es Salaam na Mradi wa kopa kuku lipa kuku katika Kata ya Miteja, Kilwa, mkoani Lindi.
Alisema kuwa hivi sasa Namaingo tayari imewafikia wananchi 400,000 nchi nzima ambapo 10,000 kati ya hao wamweza kujiunga na kukidhi vigezo vya kuwa wanachama.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi hati Mwenyekiti wa Bodi ya Ushirika wa Namaingo Vibidar, Ubwa Ibrahim. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Ushirika wa Vikundi vya Biashara (Vibidar Namaingo), Wilaya ya Kinondoni, Loiruck Mollel katika sherehe iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo, Ubwa Ibrahim. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Mashingo akihutubia wakati wa sherehe hizo
Wanachama wa Vibidar wakisikiliza kwa makini hotuba
Mashingo akitia saini kwenye vyeti vya ushirika alivyovikabidhi Vibidar
Wanachama wa Vibidar Namaingo wakiwa katika sherehe hiyo
Msanii akihutubia wakati wa sherehe hiyo
Mkurugenzi wa Shitindi Poutry Farm, Shitindi akielezea kuhusu ununuzi wa mayai na kuku ambayo yeye atakuwa ndiyo mteja kutoka kwa wanaushirika
Zaituni Mchata kutoka NSSF akielezea ushirikiano uliopo na Namaingo
Ofisa wa NMB, Philimon Komu akielezea fursa za mikopo zilizopo katika benki hiyo
Ofisa wa Benki ya CRDB Tawi la Banana, Anjela Mramba akiwakaribisha wanachama wa Vibidar Namaingo kufungua akaunti na kukopa kwenye benki hiyo
Lobulu akifurahia kupata cheti cha ushirika
Lobulu akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Vibidar Namaingo, Ubwa Ibrahim
Mwenyekiti wa Vibidar Namaingo Wilaya ya Temeke, Regina Mutainulwa (kushoto) akipongezwa na wanachama baada ya kukabidhiwa cheti cha ushirika.
Ni furaha iliyoje
Lobulu akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu, Mashingo
Ubwa akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mashingo
Mashingo na Ubwa wakielekea kukagua bidhaa za wajasiriamali wanachama wa Vibidar Namaingo
Mashingo akinunua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali
Bi Ubwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vibidar Namaingo
No comments:
Post a Comment