Thursday, February 16, 2017

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AFANYA ZIARA JIMBONI,ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA DARAJA LA GALAMBA

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Februari 15,2017 ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia miundo mbinu iliyopo katika jimbo hilo. 

Siku ya kwanza ya ziara ya mbunge huyo ilikuwa katika kata ya Kolandoto,Ibadakuli,Shinyanga Mjini,Kambarage na Ngokolo. 
Mheshimiwa Masele alikuwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga. 
Mheshimiwa Masele ametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ambalo lipo kati mto mkubwa maarufu kwa jina la ‘Mto Simba’. 
Mbunge huyo pia amejionea jinsi barabara ya kutoka barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza kwenda hospitali ya Kolandoto ilivyokatika na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Kolandoto. 
Ziara ya Mbunge Masele pia ilifika katika masoko makubwa yaliyopo katika jimbo hilo ikiwemo soko la Kambarage lililopo kata ya Kambarage,Nguzo Nane lililopo kata ya Shinyanga mjini,soko kuu la mkoa wa Shinyanga na soko la Mitumba maarufu ‘Ngokolo Mitumbani’ lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga. 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika ziara hiyo ametuletea picha 44 za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele.
Hapa ni katika Barabara ya Kolandoto- Wami ambayo inatoka katika barabara kuu ya Shinyanga- Mwanza-Kushoto ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akimuonesha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele (wa pili kushoto) jinsi barabara hiyo ilivyomong’onyoka hali inayotishia kukatika kwa barabara hiyo inayoelekea katika hospitali ya Kolandoto.
Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni katika Ofisi ya CCM Kata ya Kolandoto-Aliyesimama ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza wakati akimkaribisha mheshimiwa Masele aweze kuzungumza na baadhi ya wananchi wa kata hiyo huku akibainisha kuwa ziara hiyo inalenga kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Diwani wa Kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya ambaye pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga akielezea changamoto ya gharama kubwa za matibabu katika hospitali ya Kolandoto hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo wakose huduma ya afya kama inavyotakiwa matokeo yake kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo katika kituo cha Afya Kambarage au Zahanati ya Galamba.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto ambapo alisema ziara hiyo siyo ya siasa bali ni kiutendaji.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alieleza kukerwa na changamoto ya gharama kubwa ya matibabu katika hospitali ya Kolandoto na kuahidi kuzungumza na mamlaka zinazohusika ili kumaliza tatizo hilo.Mheshimiwa Masele pia alisema serikali/Chama Cha Mapinduzi kinafanya jitihada zote ili kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya Kolandoto wanapata huduma ya maji safi na salama.
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akimwelezea Mheshimiwa Masele changamoto zilizopo katika kata hiyo
Mkazi wa Kolandoto Kadesha Noniyaza akielezea kero ya maji katika kijiji cha Wami na Mwanubi 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi katika Senta ya kijiji cha Galamba kilichopo katika kata ya Kolandoto baada ya kumuomba asimame wamwelezee changamoto zinazowakabili ambazo ni maji na uhitaji wa daraja katika mto Simba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wananchi hao na kuwaeleza namna serikali inavyojitahidi kuhakikisha kuwa kero zao zinamalizika
Hapa ni katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka 2017.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia daraja hilo ambalo mpaka kukamilika kwake jumla ya shilingi milioni 429.8 zinatarajiwa kutumika. 
Mmoja wa wataalam katika ujenzi huo akimwelezea mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele namna ujenzi huo unavyoendelea. 
Daraja hilo lina urefu wa mita 26 na upana wa mita 8
Ujenzi wa daraja ukiendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishindilia zege kwa kutumia mashine kwenye daraja hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza kwenye daraja la Galamba ambapo alisema ujenzi huo wa daraja ambalo litaboresha mawasiliano katika kata ya Kolandoto na manispaa ya Shinyanga kwa ujumla ni miongoni mwa ahadi ambazo aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya (CCM) akizungumza ambapo alisema mradi huo unatekelezwa kupitia mfuko wa barabara 'Road Fund' huku akiongeza kuwa daraja hilo litaunganisha wilaya ya Shinyanga,Wilaya ya Kishapu na Meatu na kwamba kabla ya ujenzi huo eneo hilo lilikuwa kero hasa wakati wa masika
Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd akielezea mradi huo wa daraja ambapo alisema mpaka sasa ameshakamilisha ujenzi wa vitako vyote vya daraja na ujenzi wa kuta/nguzo zote za daraja na kwamba anaendelea kutengeneza kindanda cha daraja ya upande mmoja na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 75.
Muonekano wa daraja hilo
Ujenzi unaendelea
Muonekano wa daraja na eneo ambapo mto Simba unapita
Mheshimiwa Masele akiteta jambo na Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd
Hapa ni katika Shule ya Msingi Bugweto iliyopo kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga-Wanafunzi na walimu wakimpokea mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akimtambulisha Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri (katikati) na diwani wa kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya (CCM) ambaye pia naibu meya wa manispaa ya Shinyanga
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Bugweto na kuwataarifu wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuwa ametoa mifuko 100 ya saraji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambayo yamechakaa na hayana sakafu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto
Darasa likiwa lina kokoto na vumbi sakafuni
Hapa ni katika Soko la Kambarage kata ya Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasili katika soko hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisalimiana na mfanyabiashara katika soko la Kambarage katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Kambarage na kuwaeleza kuwa serikali ina mpango wa kujenga upya soko hilo hivyo kuwaomba wafanyabiashara wakae na viongozi wao na manispaa ya Shinyanga waangalie eneo ambalo litatumika wakati wakipisha ujenzi wa soko hilo pia kuangalia mazingira mazuri ya wafanyabishara hao kurudi na kuendelea na biashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiteta jambo na katibu wa soko la Kambarage Daudi Kitila( wa kwanza kulia)
Hapa ni katika eneo la Stendi Mpya ya Mabasi Mjini Shinyanga ambapo ujenzi wa choo cha stendi hiyo unaendelea.Katikati ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akielezea ujenzi wa mfumo wa majitaka unaoendelea katika eneo hilo
Hapa ni katika soko la Nguzo Nane kata ya Shinyanga Mjini-Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza na kujibu kero za wafanyabishara katika soko hilo.Kero kubwa iliyotolewa ni ushuru mkubwa kwa mazao ambapo Masele aliahidi kukutana na uongozi wa manispaa ya Shinyanga kufuatilia kero hiyo na namna ya kuitatua
Ndani ya Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga.Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo,kero kubwa ikiwa ni soko hilo kukosa wateja kutokana wafanyabiashara na wateja kukimbilia katika soko la Nguzo Nane na Kambarage
Hapa ni Ngokolo Mitumbani,kwenye soko la Mitumba lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.Mheshimiwa Mbunge akishangaa namna mabanda yalivyo wazi kutokana na wafanyabiashara kukimbia soko hilo na kufanyia biashara zao katika maeneo mengine mjini Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Mitumba,maarufu Ngokolo Mitumbani katika kata ya Ngokolo.
Mfanyabiashara wa Mitumba akielezea jinsi soko hilo lilivyokosa wafanyabiashara kutokana serikali kuruhusu masoko kila mahali mjini Shinyanga
Vibanda vikiwa havina nguo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akijadiliana na wafanyabiashara hao namna ya kurudisha wafanyabiashara waliokimbia 
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments: