Saturday, February 4, 2017

KONGAMANO KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako Ijumaa Februari 03, 2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga  lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Mwandishi wetu Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kongamano hilo lililoanza majira ya saa 11:25 jioni na kumalizika saa 4:06 usiku…Tazama hapa chini
Kushoto ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa Februari 3 2017 Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Sekretariati wakiwa ukumbini
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa kuendelea kufanya biashara
Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Mwalimu wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
Mkuu huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga
Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
Tunafuatilia kinachoendelea
Kulia ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama wanavyokubaliana na benki 
Pamui alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
Mkurugenzi wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha moramu 
Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
 Katibu wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo
Afisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua

Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

No comments: