Leo Jumamosi Februari 11,2017 kumefanyika kongamano kubwa la Maalum la Maombi kwa Wanavyuo mkoani Shinyanga.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa vyuo na dini,wanakwaya,wanafunzi wa shule za sekondari na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Shinyanga limetokea baada ya Mtumishi wa Mungu Happiness Mwaja Kihama kutamani kuwepo kwa kongamano ndipo wanafunzi kwa pamoja wakakubali kuunganisha nguvu hatimaye kufanikisha kufanyika kwa kongamano hilo.
Miongoni mwa malengo ya Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa –Mithali 1:7”ni kuwaleta pamoja wanafunzi na kuwafanya wafahamiane,kuunganisha nguvu katika kumuomba mungu kwa ajili ya kuendelea ustawi wa kielimu katika mkoa wa Shinyanga.
Pamoja na kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu,kongamano hilo pia lililenga kuwaombea wanafunzi ili mungu awasaidie kufanya vizuri katika masomo yao sambamba na kuwajengea uwezo vijana uwezo wa kumjua mungu na kusababisha hofu ya mungu ndani yao ili kuisadia serikali katika kupunguza vitendo viovu katika jamii.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametusogezea picha 50 za matukio yaliyojiri Mwanzo mpaka Mwisho..Shuhudia hapa chini
Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiweo Shycom,Mocu ,wakiwa ukumbini wakati wa kongamano Maalum la Maombi kwa wanavyuo
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza wakati wa Kongamano hilo ambapo alisema ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Shinyanga.Mchungaji Mosha aliwasisitiza vijana hao kumtanguliza Mungu katika maisha yao
Shija Simon akisoma risala ambapo alisema wameamua kukutana pamoja ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kumuomba mungu kwani wanaamini kuwa maomi hayo yatasababisha mabadiliko ya kielimu mkoani Shinyanga kwani ukilinganisha na mikoa mingine mkoa wa Shinyanga bado upo chini kielimu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mchungaji Emmanuel Mboje wakiwa ukumbini wakati wa kongamano hilo
Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness Mwaja Kihama ambaye ni mlezi wa wanafunzi walioandaa kongamano hilo akizungumza ukumbini jinsi alivyopata maono na kuamua kuhamasisha wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga kupitia kwa wakuu wa wakuu wa vyuo kuungana ili kufanikisha kongamano hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza kwa makini mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama
Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness Mwaja Kihama alisema lengo la kongamano hilo ni kutengeneza umoja wa wanavyuo mkoani Shinyanga,kuomba kwa ajili ya elimu mkoani humo na kuwaombea wanafunzi wote mkoani Shinyanga
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa somo kuhusu "Funguo za Kiagano za Kupata Majibu ya Maombi yetu"
Wanafunzi wa vyuo wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kutoa somo ambapo aliwataka wanafunzi kumtegemea mungu ili kufanikiwa katika masomo na maisha yao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwapongeza wanafunzi hao kuungana pamoja kuuombea mkoa wa Shinyanga kwani yatasababisha wawe na hofu ya mungu ili kusaidia kupunguza vitendo vya uovu katika jamii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wanafunzi hao kujitahidi kusoma na kuachana na tamaa zisizofaa
Mchungaji Goodluck Mosha akiomba ukumbini wakati wa kongamano maalum la maombi kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga
Wanakwaya ya Haleluya kuu ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga wakicheza ukumbini
Uimbaji unaendelea
Wanachuo wakiimba na kucheza
Vijana wakicheza
Kijana Gabriel akiimba
Vijana wakimwimbia bwana
Uimbaji unaendelea
Wanavyuo wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Wanachuo wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Wanachuo wakiimba ukumbini
Vijana wa TYCS wakiimba ukumbini
Washiriki wa kongamano hilo wakicheza ukumbini
Kongamano linaendelea
Tunafuatilia kinachoendelea
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiongoza maombi kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu kwani hali ya kitaaluma ipo chini ukilinganisha na mikoa mingine
Wanafunzi wakiwa wamenyoosha mikono wakati wa maombi
Washiriki wa kongamano wakiwa wamenyoosha mikono
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiomba wakati wa kongamano hilo la maombi maalum kwa wanafunzi wa vyuo vya mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akiwa katika maombi
Maombi yanaendelea
Wanafunzi wakiwa katika maombi
Maombi yanaendelea
Maombi yanaendelea
Maombi yakiwa yamekolea kuombea mkoa wa Shinyanga
Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiendelea kuomba
Maombi yanaendelea
Maombi yakiendelea
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiombea wanafunzi wa vyuo na wanafunzi wa shule za sekondari waliohudhuria kongamano hilo
Maombi yanaendelea
Wanachuo wakiendelea kumsifu bwana Yesu kwa nyimbo
Kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Kongamano hilo Jepherson Jackson akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo ambapo aliwashukuru watu wote waliofanikisha kongamano hilo na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na mlezi wao Happiness Mwaja Kihama ili kuandaa kongamano jingine
Mchungaji Emmanuel Mboje akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo ambapo aliwataka wanafunzi hao kupendana na kuhakikisha wanakwenda kusali na kumuomba mungu
Picha ya pamoja mgeni rasmi na kamati iliyofanikisha kongamano hilo
Kamati iliyofanikisha kongamano hilo ikiongozwa na mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama ambaye pia ni mkurugenzi wa EasyFlex Production wakiwa katika picha ya pamoja baada kumalizika kwa kongamano hilo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment