SIMU.TV: Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa makosa manne ya uchochezi yanayomkabili. https://youtu.be/IwDGQgmwVwc
SIMU.TV: Msanii maarufu wa filamu nchini Wema Sepetu na wafanyakazi wake wa ndani wawili wamefikishwa mahakani leo na kusomewa mashtaka yanayo wakabili ya kukutwa na msokoto wa bangi. https://youtu.be/EXrjv7yu10k
SIMU.TV: Baraza la viongozi wa dini lakupambana na dawa za kulevya limesema linaunga mkono vita ya kupambana na madawa ya kulevya inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. https://youtu.be/z_L1I1xv934
SIMU.TV: Zaidi ya shilingi bilioni 40 zinatarajiwa kutumika katika uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa zinazotokana na mmea aina ya shubiri hapa nchini. https://youtu.be/zCPhCQaTTCo
SIMU.TV: Baadhi ya wafanyakazi wa maduka ya vifaa vya ofisini na mashuleni wamezungumzia kadhia wanayoipata kutokana na kuenea kwa biashara ya wino bandia hapa nchini. https://youtu.be/SSEgtza3mV4
SIMU.TV: Jamii imekumbushwa umuhimu wa kuwania kupata elimu ya juu ili kuweza kuongeza ujuzi na ufanisi katika fani mbalimbali hapa nchini. https://youtu.be/Zs25xZFnuHw
SIMU.TV: Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili watu saba akiwemo afisa wa mamlaka ya mapato TRA imetajwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Mbeya. https://youtu.be/WE6aO0MNu6g
SIMU.TV: Serikali ya Uholanzi imeingiza aina kumi na nne ya mbegu za viazi hapa nchini ikiwa ni juhudi za kuboresha uzalishaji wa zao hilo kwa manufaa ya mkulima. https://youtu.be/LD7IYO09Da8
SIMU.TV: Mkoa wa Ruvuma umeingia makubaliano ya kibiashara na wilaya tatu za nchini Malawi ikiwa ni juhudi za kuongeza fursa za biashara kwa wafanyabiashara wa mkoa huo. https://youtu.be/SHe4g_PM1zI
SIMU.TV: Vijana wilayani Kilombero mkoani Morogoro wameshauriwa kuunda vikundi na kuvisajili ili waweze kunufaika na mikopo kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri hiyo. https://youtu.be/32TVrGdEzJg
SIMU.TV: Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga leo wamefurika katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam ili kushudia hatma ya mwenyekiti wa klabu yao Yusuf Manji aliyeitwa kwa mahujiano kuhusu tuhuma za madawa ya kulevya. https://youtu.be/L76328l49Fs
SIMU.TV: Uchaguzi wa viongi wa chama cha michezo cha Tenisi unatarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ofisi za baraza la michezo BMT. https://youtu.be/gGALcMFkhSQ
SIMU.TV: Shirikisho la soka bara la Ulaya UEFA lina mpango wa kuwasilisha pendekezo la kupeleka timu kumi na sita kutoka barani humo katika mashindano ya kombe la dunia kuanzia 2026. https://youtu.be/o_R6pf55egs
No comments:
Post a Comment