Wednesday, February 15, 2017

BANKI YA CBA TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO VALENTINE DAY PAMOJA NA WATEJA WAO

Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania, Gift Shoka ( kushoto) akisaidiwa kukata keki na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja wa benk hiyo,Hyasinta Mwimanzu wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wapendanao duniani ambapo benki hiyo iliadhimisha siku hiyo pamoja na wateja wao(hawapo pichani) katika . makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Ssalaam jana.
Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania, Gift Shoka ( kushoto) akimlisha keki mmoja wa wateja wa benki hiyo ambaye ni Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Britan Insurance ( T) Limited, Farai Dogo wakati wa kuadhimisha siku ya wapendanao duniani(Valentine’s Day) ambapo wafanyakazi wa benki hiyo walishirikiana na wateja wao kuadhimisha siku hiyo muhimu duniani kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam jana.
Baadhi ya wateja wa benki ya CBA Tanzania pamoja na wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Benki hiyo, Gift Shoka ( kulia) wakati wa hafla fupi ya kusherehekea siku ya wapendanao duniani pamoja na wateja wa benki hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania, Gift Shoka ( kushoto) akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Maria Shawa wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wapendanao ambapo benki hiyo iliadhimisha siku hiyo pamoja na wateja wao katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Wateja wa benki ya CBA Tanzania , pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Benki hiyo, Gift Shoka(katikati) mara baada ya kukata kula keki ikiwa ni ishara ya kuadhimisha siku ya wapendanao duniani leo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments: