Nasieku
Kisambu Mkurugenzi wa Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA)
akizungumza katika mafunzo ya Haki za Wanawake na Jinsi ya kufanya
utetezi katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yakiwa na lengo
la kuongeza uelewa wa misingi ya kulinda na kutetea haki za wanawake na
watoto Kitaifa , Kikanda na Kimataifa.
Kuelewa
mifano iliyopo katika Kanda, Kikanda na kimataifa inayolinda haki za
wanawake , Haya ni mafunzo yanayolenga kujenga uwezo wa Taasisi
zinazotetea haki za wanawake kutumia fursa zilizopo katika mikataba,
Taasisi na mifumo ili kuweza kubadilisha sera na sheria kandamizi na
kutetea haki za wanawake.
Mafunzo
hayo yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es
salaam yameandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na
kwa ushirikiano na mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na
watoto ambapo wadau mbalimbali kutoka katika taasisi hizo wameshiriki
katika mafunzo hayo
Maria
Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania
(TAWLA) akifungua mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika kwenye hoteli
ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
Mkufunzi
wa Mafunzo hayo Dk. Clemence Mashamba akitoa mada wakati wa mafunzo
hayo yanayoendelea kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es
salaam.
Christina
Kamili Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And
Providers akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo
hayo Dk. Clemence Mashamba hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa kititolewa na mkufunzi huyo.
Christina
Kamili Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And
Providers akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo
hayo Dk. Clemence Mashamba hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
Mkufunzi
wa mafunzo hayo Dk Clemence Mashamba akiwa na Dotto Joseph Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya National Oganization For Legal Assistance
(Nola)
Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania TAWLA akipitia nyaraka za mmbalimbali za mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment