Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati)
akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi
la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya
Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika
jimbo la Dimani leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles
Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya
Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni
katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya Upigaji wa Kura leo.
Mmoja
wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika
jimbo la Dimani leo.
Baadhi ya
Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali
wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.
Mmoja
wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika
jimbo la Dimani leo.
Wananchi
wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura katika kituo cha Bweleo katika
jimbo la Dimani leo.
Picha
na Aron Msigwa –NEC.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Kushoto)
akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo ndani ya kituo cha
kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani leo. Wengine wanaochukua
taarifa ni Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Na. Aron Msigwa – NEC,
Zanzibar.
22/1/2017.
Hatimaye wananchi wa
Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua
Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.
Zoezi la upigaji wa
Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1 asubuhi likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku
baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri
yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC) kufanikisha Uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza kuhusu
mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo hilo na kuzungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo
vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali
vya kupigia Kura.
“ Viongozi wa Tume tumetembelea
vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la Dimani; tumeona wenyewe
upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi
wa Vituo vya Uchaguzi kila mmoja amesema
Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani
unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.
Amesema Wasimamizi wa
Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto zilizokuwa
zikijitokeza katika baadhi ya vituo vya
kupigia Kura.
Ameeleza kuwa zoezi
zima la upigaji wa Kura linaendeshwa kwa uwazi mkubwa, Utulivu na Amani na
kuwawezesha wananchi kupiga kura bila vikwazo vyovyote.
Aidha, Mhe. Kaijage
amebainisha kwamba endapo yatajitokeza malalamiko yoyote wakati zoezi la
upigaji wa Kura likiendelea katika vituo mbalimbali , Mawakala wa Vyama vya
Siasa ambao ni wasimamizi wa Maslahi ya Wagombea na Vyama vyao Vituoni watajaza
fomu ya malalamiko Na. 14 kwa mujibu wa Sheria ambayo inatoa
fursa ya kushughulikiwa kwa malalamiko hayo.
Aidha, amebainisha kuwa
mara baada ya zoezi la upigaji wa kura kumalizika leo saa 10 jioni kazi ya
kuhesabu Kura itafuata ili hatimaye wamnanchi wa Jimbo la Dimani waweze
kupatiwa matokeo ya maamuzi waliyoyafanya kupitia Kura zao.
Mhe. Kaijage
amesisitiza kuwa Wasimamizi wote wa Uchaguzi huo wamepewa mafunzo ya kuzingatia
ili kuhakikisha wanaendesha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa na kuwezesha matokeo
kutangazwa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kumjua mshindi wa Uchaguzi huo.
“ Endapo taratibu
zote za Uchaguzi zitakuwa zimekamilika kwa mujibu wa Sheria, hakutakuwa na
sababu yoyote ya kuchelewesha matokeo,mpaka sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi tumeridhishwa
na mwenendo mzima wa zoezi la upigaji wa Kura na matokeo yatatolewa kwa wakati”
Amesisitiza.
Kwa Upande wake
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel
Kawishe akizungumzia zoezi la Upigaji wa Kura amesema kuwa Wapiga Kura
wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliokidhi Sifa na Vigezo vilivyoainishwa
kisheria kuwawezesha kupiga Kura.
Amesema kwa mujibu wa Sheria Msimamizi wa Kituo ndiye
mwenye mamlaka ya maamuzi katika kituo cha kupigia Kura ikiwa ni pamoja na
kuamuru kuondolewa kwa mtu yeyote atakayeonekana kufanya fujo au kuzuia zoezi
la uchaguzi kuendelea kituoni.
Katika Uchaguzi Uchaguzi huo mdogo wa Ubunge wa
jimbo la Dimani jumla ya Wapiga Kura 9,280 wanatarajiwa Kupiga kura katika
Vituo 29 huku vyama vya Siasa vyenye wagombea vinavyoshiriki Uchaguzi huo ni 11
huku Waangalizi wa Uchaguzi waliojitokeza kushiriki katika Uchaguzi huo ni
zaidi ya 300.
No comments:
Post a Comment