Friday, January 27, 2017

Tume ya Mipango kuanza Safari ya kuhamia Dodoma Mwezi Machi

Na Adili Mhina, DSM.
Katika kuitikia na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume ya Mipango inatarajia kuanza kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau Makuu ya Nchi ifikapo mwezi Machi Mwaka huu. 
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipokutana na watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari 26, 2017 kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo.
Pamoja na agenda zingine kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia Dodoma lilionekana kuchukua nafasi kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara baada ya ratiba ya zoezi hilo kutolewa rasmi ambapo wengi walionesha kufurahishwa na kutendo cha kutimiza ahadi ya Rais kwa wananchi ya kuhamia Dodoma.
Mwanri alieleza kuwa Tume ya mipango itahamisha watumishi wake katika awamu tatu ambapo makundi mawili yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka huu.
“Kundi la kwanza kwa upande wa Tume ya Mipango litaondoka mwezi Machi mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine, watumishi wa kundi hili watakuwa na jukumu la kuandaa mazingira kwa ajili ya kuwapokea watumishi wengine watakaohamia baadae,” alisema Mwanri. 
Aliongeza kuwa sehemu ya  pili ya watumishi inatarajiwa kwenda Dodoma kuanzia mwezi Septemba mwaka huu ambapo pamoja na watumishi wengine, kundi hilo linajumuisha Mkuu wa Taasisi ambaye ni Katibu Mtendaji akiambatana na Wakuu wa Klasta, Idara pamoja na Vitengo na kundi la mwisho linatarajiwa kuhama kuanzia mwezi Machi, 2018.
Kikao hicho pia kilitoa fursa ya kutolewa kwa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2016/17. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah alieleza kuwa katika Kipindi hicho Tume ya Mipango imefanikiwa kutekeleza majukum mbalimbali ikiwemo;  kuandaa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18na kuendesha mafunzo kuhusu mwongozo wa usimamizi wa Uwekezaji wa Umma  katika ngazi ya Sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa nchini. 
Mafanikio mengine ni kuendelea kusambaza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) kwa wadau pamoja na kuendelea kuandaa mikakati minne ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaendelea (Mkakati wa utekelezaji, Ugharamiaji, Mawasiliano na Ufuatliaji na Tathmini). 
Aidha Tume ya Mipango ilifanikiwa kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Tabora, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es salaam kwa lengo la kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi na kuelewa changamoto zinazokabili utekelezaji wa miradi hiyo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri Akiongea na watumisi wa Tume ya Mipango (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akifuatiwa Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiongea jambo na Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy wakati wa mkutano na watumishi wa taasisi hiyo.

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2016/17.
 Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akiwasilisha mada juu ya maadili kwa watumishi wa umma katika mkutano uliowahusisha wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
  Mwanasheria wa Tume ya Mipango, Bibi Nyanzala Nkinga akichangia jambo katika mkutano wa wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
 Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
 Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
 Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
 Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
 Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.

No comments: