Wednesday, January 25, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


Benki ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam. https://youtu.be/CTR6pEcZenM

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kuangalia mwenendo wa vyama vya ushirika nchini ili kuwawezesha wakulima kunufaika na vyama hivyo. https://youtu.be/L-q7LgWHcIM

Watu wanne wakazi wa kata ya Oldonyo Sambu wilayani Arumeru wameuawa baada ya kutokea majibizano ya risasi na askari wa hifadhi ya Arusha katika tukio la kuzuia wasiingize mifugo katika hifadhi hiyo. https://youtu.be/3As4_TxEEvw

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya jengo lilokuwa likijengwa mjini Unguja kuporomoka. https://youtu.be/lnJsbE0hRko
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Willium Lukuvi ameonya kuzivunja serikali za vijiji zitakazo bainika kuvuruga mpango wa matumizi bora ya ardhi. https://youtu.be/fA1DH-5DP1g

Serikali imesema baadhi ya wanasheria katika halmashauri mbalimbali nchini wamekuwa kikwazo katika kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya ardhi. https://youtu.be/T9gcWZs12-0

Serikali mkoani Kagera imepiga marufuku uingizwaji wa mifugo jamii ya ndege katika mkoa huo kutoka nje ya nchi bila kibali cha wizara. https://youtu.be/DxFi9p4OuxQ

Wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji Zanzibar imelitaka shirika la nyumba la Zanzibar ZHC kujiendesha kibiashara ili kuboresha huduama zake. https://youtu.be/5xHq8oDt87g

Kampuni ya uwekezaji ya chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA imetangaza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es Salaam ili kupata mtaji wa kuendeleza miradi yake. https://youtu.be/ROw_te4kSU4

Baadhi ya wajasiriamali mkoani Kilimanjaro wamelipongeza shirika la Forester Tanzania kwa kuwapa elimu ya kupanda miti katika vyanzo vya maji. https://youtu.be/pMW7sriQ7R8

Kamati ya rufaa ya TFF imesema itakaa kusikiliza na kutolea uamuzi rufaa ya timu ya Polisi Dar es Salaam inayo lalamikia timu ya Simba kumchezesha mchezaji mwenye kadi nyekundu. https://youtu.be/aH646JngDRw

Timu ya Azam Fc imesema wembe iliotumia kuinyoa Simba kwenye michuano ya kombe la mapinduzi itautumia tena kuinyoa mwisho wa juma kwenye mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara. https://youtu.be/mDSOwREoYv0

Bingwa  mara sita wa michuano ya tenisi ya Australia open Serena Williams ametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. https://youtu.be/oixaQk-MaiA

No comments: