Friday, January 20, 2017

SEMINA YA MAFUNZO YA KARATE KIMATAIFA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA


Wakufunzi wanaoingia kufanya mtihani wa kupandishwa madaraja wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza maelekeo kabla ya kuanza kufanya mtihani huo.

Wakwanza kushoto ni Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree ambaye ni raisi wa shirikisho la West Shotokan Karate Internation duniani ,akifuatiwa na Mkufunzi wa West shotokan Karate Kanda ya kaskazini Dady K.Ramadhan.
Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan akiwa anawapa maelekezo wakufunzi wanaofanya mtihani wa kupanda madaraja kabla ya darasa kuaza rasmi .
Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan degree akiwa tayari kuanza kuwafanyisha mtihani wakufunzi ambao wanahitaji kupanda madaraja .

wakufunzi wakiwa wanaendelea kufanya mtihani kwa njia ya vitendo mbalimbali ili waweze kupanda madaraja.
Wakwanza kushoto Mkufunzi Hamis Abdallah akiwania Dan ya nne ,akifuatiwa na aliyepo katikati Sensei Taifa Liwewa naye akiwania Dan ya nne.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakwanza kushoto ni sensei Hamis Wembo kutoka mkoani Kilimanjaro pamoja na Sensei Ally Iddy kutoka mkoani Arusha wakifanya mtihani wa kuwania Dan ya tatu kwa mujibu wa west Coast Shotokan Karate ASSN.

Wakwanza kushoto Mkufunzi Hamis Abdallah akiwania Dan ya nne ,akifuatiwa na aliyepo katikati Sensei Taifa Liwewa naye akiwania Dan ya nne,na wa kwanza kulia ni sensei Dady K.Ramadhan akiwania Dan ya tano.Picha na Vero Ignatus Blog. 
Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree baada ya kumaliza kufanya mitihani kwa vitendo katika hatua mbalimbali .

Afisa michezo wa jiji la Arusha Mwamvita Okong'o ,akiwa pamoja na Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno akipokea zawadi kutoka kwa rais wa shirikisho West Shotokan Karate Internation duniani kwa Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree

Wapili kushoto ni Afisa michezo wa Mkoa wa Arusha Mwamvita Okong'o ,walieko kulia kwake ni Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo katikati ni muwakilishi kutoka kampuni ya Benson ,akifuatiwa na Master Shihan Shalom Avitan na wa kwanza kulia ni Sensei Dady K.Ramadhan.
Sensei Taifa Liwawa akikabidhiwa cheti cha kuwa Master of Art wa 27 katika  shirikisho hilo ulimwenguni mwote .Picha na Vero Ignatus Blog

Mmoja wa wakufunzi Ally Iddy akipokea cheti kwa kufaulu kuingia Done ya tatu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Mafunzo ya karate ya kimataifa yanayoambatana na kufanya mtihani wa kupanda madaraja yamefanyika Jijini Arusha yakiongozwa na Master Shihan Shalom Avitan, kutoka nchini Israel .

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa michezo mkoa wa Arusha Mwamvita Okeng’o ambapo amesema kuwa serikali imeipa michezo kipaumbele ili kupunguza tatizo la ajira nchini na amewataka wanamichezo hao kuuambikiza katika jamii kwa ujumla

Akijibu risala iliyoandaliwa na West coast Shotokan internation Karate( ASS'N) Afisa michezo huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inafanya jitihada ili kuwapatia eneo la kudumu la kufanyia mazowezi kama walivyoomba.

Naye afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuwa michezo  inaimarisha afya ,ni ajira hivyo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu huku akiwasisitiza vijana kutumia fursa hiyo ili waweze kujiajiri.


Muandaaji wa mafunzo hayo hapa nchini Sensei Dady Ramadhan ambaye ni Mkufunzi kiongozi amesema kuwa wapo wanakarate wanaocheza Shotokan ambao wana daraja mbalimbali katika taaluma hiyo miongoni mwao wapo waliofanya mtihani na wamepanda daraja

Aidha amesema kila mwaka wanamuita mwalimu na kufanya mitihani ,hivyo amewataka wale wote wanaotaka kuifunza mchezo huo wahakikishe wanajicfunza kupitia wataalamu ambao wamepitia mafunzo hayo na wenye uzoefu wa kutosha.

“Unajua kwa sasa mchezo huu unawaalimu wengi ambao wamevamia hawana taaluma kabisa hivyo msikubali kuburuzwa na kufundishwa na hao watawapotosha na kuleta madhara kwani hawazifahamu kanuni na miiko ya karate.”alisema sensei Dady.

Kwa upande wake sensei Taifa Liwewa ambaye ni Katibu wa shirikisho West Coast shotokan Karate ambaye kitaaluma ni msanifu jukwaa(Stage Craft designer amesema kuwa karate siyo mchezo wa kihuni wala wa watu wasio na elimu bali nimchezo wa watu wote.

“kuna watu wananishangaza sana wanadhania kuwa watu wote waliokuja kucheza karate ni watu wasiokuwa na elimu,wahuni,siyo kweli mimi nimezaliwa nikaikuta karate nyumbani kwetu,mama yangu mzazi ana miaka 70 lakini bado anacheza karate ,baba yangu alikuwa naye anacheza ,kaka yangu vilevile ,mimi mwenyewe natamani watoto wangu wacheze karate.”alisema sensei Taifa.

Amesema kuwa karate ina sheria na taratibu zake ,ameongeza kuwa mchezo huo wenye maadili,nidhamu,utiifu pamoja na uadilifu kwani unajenga mwili na kuimarisha afya,amesema zipo nguzo 5za mazowezi,nguzo 9 za mafunzo, pamoja na miiko ya karate 20.

Wakufunzi walioshiriki katika kufanya mtihani idadi yao walikuwa 13 kutoka Arusha,Kilimanjaro 1,Dar es salaam 4 na imeshirikisha vilabu vitano,mafunzo hayo yalikuwa ya siku tatu kuanzia 18januari hadi 20 januari

Mafunzo hayo yamefungwa rasmi na mwenyekiti wa chama cha karate mkoa wa Arusha Sensei Dady K.Ramadhani,ambapo amesema kuwa mafunzo ya mwaka huu yamekuwa mazuri na wanafunzi wamefanya mtihani kwa ufahaulu wa hali ya juu,mafunzo kama haya yanatazamiwa kufanyika tena januari 2018

No comments: