Tuesday, January 10, 2017

RC MAKALLA AKUTANA NA VIONGOZI NA WANAFUNZI WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA, VIONGOZI NA WADAU WA SOKA MKOA WA MBEYA

Image may contain: 20 people, people standing

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla  amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi na kuwaeleza mambo mbalimbali ikiwemo hali ya usalama, shughuli za kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Mbeya 

Amewaeleza kwa takwimu za kiuchumi Mkoa wa Mbeya ni Mkoa wa Tatu kwa kuchangia pato la Taifa baada ya Dar es salaam na nwanza 

Viongozi wa Chuo na wanafunzi wamefurahishwa na jitihada za serikali ya Mkoa kudumisha amani na kwa kufanya hivyo wananchi kushiriki kikamilifu ktk shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Mkoa amewaeleza kuwa Siri ya mafanikio ni ushirikiano ulipo kati ya serikali na wananchi ni matumaini yake kuwa Mkoa wa Mbeya utapiga hatua katika maendeleo.
Image may contain: 15 people, people smiling, people standing
Mkuu wa Mkoa wa Meya Mh.Amos Makalla atangaza kuunda Kamati ya kusaidia timu za Mbeya 
- Achangia sh 3,000,000( milioni Tatu) kwa timu ya Mbeya Kwanza iliopo Daraja la kwanza na Mbarali United iliopo Daraja la pili 
- Awataka WADAU kushirikiana na kuepuka Makundi na Siasa katika Soka 
- Awagiza wakuu wa wilaya ,wakurugenzi na madiwani kutenga maeneo ya michezo
- Awakaribisha wadau na wawekezaji kuwekeza katika sport academy.

No comments: