MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya
kwa wakati zaidi ya bilioni 5.1 kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148.
Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa
kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko
huo .
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati
akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa.
Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka
2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa
mwaka huu.
Alisema pamoja na malipo kuongezeka
lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya
vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.
Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa
magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya.
“Lakini
changamoto nyengine ni ugonjwa wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa
nyemelezi na lakini pia halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa
tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo vyao “Alisema.
Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa
mfuko huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo
vinavyoashiria wizi na udanyanifu.
“Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa
kuokoa kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29
zilifanyika kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au
uadanyanyifu wa huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.
“Kaguzi
hizo zilifanyika kwenye vituo vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya
madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia 36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na
asilimia 19 “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangaraha
No comments:
Post a Comment