Friday, January 20, 2017

NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mst. Zanzibar, Hamid M. Hamid (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa NEC walipotembelea vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Dimani kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika Jumapili, Januari 22, 2017.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi na Msingi Dimani, Zanzibar kukagua kukamilika maandalizi ya Uchaguzi wa Ubunge katika jimbo hilo leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani bi. Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la Dimani. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa pili ), Msimamizi Msaidizi wa jimbo la Dimani Bi. Idaya Selemani Hamza (katikati), Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Orodha ya Majina ya Wapiga kura iliyobandikwa Siku nane kabla ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika kituo cha kupigia kura cha Nyamanzi chenye wapiga Kura 603 katika jimbo la Dimani leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emanuel Kawishe (kushoto) mara baada ya kukagua mabango ya Matangazo ya Tume kuhusu upigaji wa kura, Orodha ya Majina ya Wapiga kura na wagombea katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi Kisakasaka, Dimani Zanzibar leo.
Moja ya Tangazo la Elimu ya Mpiga Kura linaloonyesha utaratibu wa kufuata wakati wa kupiga Kura lililobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Kisakasaka katika jimbo la Dimani.

No comments: