Thursday, January 5, 2017

NAIBU WAZIRI JAFFO AAGIZA KUUNDWA TUME YA KUCHUNGUZA MAMILIONI YA FEDHA YALIY0TOLEWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MKURANGA



.Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Mkuranga leo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akipata maelezo ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega juu ya wananchi kulalamikia upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkuranga katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akielezwa na mgonjwa, Emiliana shila aliyefika katika Hospitali Mkuranga akiwa na vifaa Tiba na Dawa alizoambiwa akanunue nje leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo katika ziara Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Hassan Sanga akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo katika ziara Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akiwasili katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni ziara ya yake kuangalia utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mkuranga pamoja wajumbe wa Baraza la Madiwani wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani wakati ziara aliyoifanya leo. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Muonekano wa Wodi ya Wazazi Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo alifnya ziara leo .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akiwa na kitabu cha stakabadhi za malipo ambazo kwa sasa hazitumiki katika sehemu za huduma za serikali leo anaeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid (kulia).








Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kuunda Tume ya kuchunguza upotevu wa fedha za dawa katika Hospitali ya Mkuranga, Mfumo wa ukusanyasaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi.

Jaffo ametoa agizo hilo wakati alipokutana na watendaji wa Halmashauri ya Mkuranga leo, amesema serikali ilitoa sh. milioni 258 kwa ajili ukarabati wa Hospitali kati ya hiyo , Sh. milioni 86 ya kununulia dawa lakini dawa zilizonunuliwa katika Hospitali hiyo ni za sh. Milioni 22 na fedha iliyobaki haina majibu

Amsema wananchi wanahitaji dawa kutokana na fedha wanayochangia katika huduma ya afya kukosa dawa kwao suala ambalo sio matarajio yao.
Jaffo amesema kuwa ukusanyaji mapato katika hospitali ya Mkuranga sio mzuri kutokana na kutumia mfumo makaratasi ikilinganishwa na sehemu nyingine kutokana na kutumia mashine za Kieletroniki.

Amesema Hospitali ya Mkuranga inakusanya mapato ya sh. Milioni 2.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana sh. milioni 2.1 ambapo ongezeko lake ni sh. 600, 000 wakati Hospitali zingine zinakusanya zaidi ya sh. milioni 20.

Mwitikio wa kufika kwa Naibu Waziri Jaffo kulitokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ambaye alifanya ziara katika vijiji 90 na malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa dawa katika Hospiali ya Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

Hata hivyo, Jaffo ametoa agizo la Kisima cha Mwarusembe ndani ya siku tatu awe amepata majibu ya kuridhisha kutokana wananchi kukosa maji kwa muda mrefu. Nae Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema wananchi wanaweza kuondokana na tatizo la kukosa dawa kutokakana watendaji kufuata taratibu za uombaji

No comments: