Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,
Omary Kumbilamoto akizungumza na wadau
wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha ZENUFA.
Mkurugenzi
wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akizungumza na wadau wa
wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho na muonekano wa alama mpya.
Afisa
Tarafa Ilala , Edita Samson akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Ilala
wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.
Mkurugenzi
mtendaji wa bohari ya Dawa nchini(MSD), Laurean Rugambwa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.
Na Humphrey
Shao, Globu ya jamii
NAIBU Meya
wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto amewataka wenye
viwanda kulinda maslahi ya wafanyakazi kabla ya serikali kuingilia kati.
Kumbilamoto
amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya
kiwanda cha dawa cha ZENUFA kilichopo kata ya Kipawa.
“tunashukuru
kwa ujenzi wa kiwandahiki na kuweza kuongeza ajira kwa vijana wetu kama ilivyo
sera ya serikali kuwa nchi ya viwanda lakini kikubwa ninacho waomba muweze kuangalia
maslahi ya wafanyakazi kuliko kusubiri msumbuliwe na serikali”amesema
Kumbilamoto.
Ametaja kuwa
itakuwa jambo la aibu kuona mkuu wa mkoa au Meya ama Naibu Meya anakuja tena
kiwandani hapa kwa ajili ya kuja kusuluhisha mgogoro wa kiwanda na wafanyakazi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi mkuu wa boahari ya dawa nchini, Raurean Rugambwa amesema kuwa
serikali imejipanga kuakikisha inasaidina na wawekezaji wa viwanda vya dawa kwa
kuwa hakikishia uakika wa soko.
Ametajakuwa kwa
sasa serikali yako imekuwa ikiagiza dawa kwa asilimia 90% kutoka nje ya nchi
kutokana na upungufu wa viwanda vya dawa hapa nchini.
Hivyo amewataka
wawekezaji kujitokeza katika uwekezaji mpya wa viwanda vya dawa katika
mpangomaalumu wa mashirikiano na serikali(PP).
wananchi
na wadau waliofika katika uzinduzi huo wakifatilia kwa makini matukio
yanayoendelea
Mkurugenzi
wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akiwaonyesha wageni
waliofika kiwandani hapo sehemu ya kiwanda hicho ambacho kinazalisha dawa aina
ya Zenufa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam,Ramadhani
Madabida akizungumza jambo na mmoja wa watumsihi kutoka MSD waliofika katika
uzinduzi wa kiwanda hicho.
No comments:
Post a Comment