Monday, January 16, 2017

NAIBU ANASTAZIA WAMBURA APOKEA BENDERA YA TAIFA TOKA KWA MISS TEEN HERITAGE 2016 NA KUZINDUA KITABU CHA "UTAMU WA CHUNGWA SI RANGIYE"

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (katikati) akiongea na Waandishi wa habari huku akiwasisitiza Vijana kuiga mfano bora aliofanya Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya changamoto alizopitia wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya zawadi mbalimbali alizopata wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akipokea Bendera ya Taifa toka kwa Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akimpongeza Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey baada ya kupokea bendera ya Taifa toka kwake leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja Mrimbwende aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey(katikati) baada ya kupokea bendera ya Taifa toka kwake leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa jamii kusoma vitabu vinavyoandikwa na waandishi mbalimbali hususan rika la Vijana ili wapate kuelimika. Kulia ni Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza.
Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (kulia) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira yake ya kuandika kitabu kwa ajili ya lengo la kuelimisha jamii hasa Vijana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa pili kushoto) akizindua Kitabu cha “Utamu wa Chungwa Sio Rangiye” kilichotungwa na kuandikwa na Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (wa pili kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Lugha Bibi. Shani Kitogo. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (wa pili kulia) mara baada ya kuzindua kitabu cha "Utamu wa Chungwa si rangiye" leo 16 Januari, 2017.

(Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)

No comments: