Thursday, January 19, 2017

MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI

Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili ( MNH),  Profesa  Lawrence Museru  leo amekutana na wahudumu  wa  Afya  katika  hospitali hiyo pamoja na mambo mengine  amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.
Pia, mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi  ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  na baadhi ya wahudumu wa afya  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Profesa Museru  amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali , lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.

" Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora  na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana  ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.

Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda  14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo  ili kuongeza  ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo.  Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Mtemi Sufiani Baruani, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala, Leila Komba,  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Hedwiga Swai wakiwasikiliza wahudumu wa hospitali hiyo katika mkutano uliowahusisha viongozi hao. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa jengo la maabara kuu.
 Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. 
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa hospitali hiyo akizungumza na wahudumu leo katika mkutano.
  Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo, Joseph Oloch akizungumza kwenye mkutano huo leo.
 Baadhi ya wahudumu hao wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru leo.
 Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo leo. 
Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo leo.

No comments: