Mbunge wa Musoma Vijijini na muandaaji wa Mashindano ya mitumbwi Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza baada ya mashindano.
Washindani wakiendelea na mashindano ndani ya ziwa Victoria katika kata ya Etaro, Musoma Vijijini
Wananchi wa Musoma Vijijini wakishangilia wakati wa mashindano ya Mitumbwi
Timu ya International iliyoshika nafasi ya mwisho ikiwasili
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma Vijijini na Diwani wa Kata ya Mugango, Charles Magoma (kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa kwanza.
Vijana kutoka Kata ya Suguti ambao walishika nafasi ya Tatu wakishangilia mara baada ya mtumbwi wao kuwasili
Mashindano
ya Mitumbwi Musoma Vijiji yaliyoshirikisha Kata 12 yamemalizika kwa Kata ya
Etaro kuibuka na ushindi na hivyo kujinyakulia fedha tasilimu milioni moja
pamoja na kombe.
Mashindano
hayo yaliandaliwa hivi karibuni na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter
Muhongo kwa ajili ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 ambapo washindi
wa pili ambao ni Kata ya Nyakatende walijinyakulia shilingi 750,000 na washindi
wa tatu ambao ni Kata ya Suguti kujinyakulia shilingi 500,000 na huku
wanaofuatia walipata shilingi 20,000 kwa kila Kata.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma Vijijini na
Diwani wa Kata ya Mugango, Charles Magoma, alimpongeza Profesa Muhongo kwa kuanzisha
mashindano ya namna hiyo jimboni humo kwani yamekutanisha wananchi wa Musoma
Vijijini kutoka pande mbalimbali za jimbo hilo.
Aliongeza
kwamba mashindano hayo yameleta mwamko mkubwa miongoni mwa vijana hasa
ikizingatiwa kuwa hakuna mashindano ambayo huwakutanisha vijana kwa wingi kama
ilivyokuwa kwa mashindano hayo ya mtumbwi.
Kwa
upande wake, mbunge wa jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo alisema aliamua
kuandaa mashindano hayo na mengine ya ngoma za asili na kuimba kwaya ili
kuwakutanisha wanamusoma vijijini kwa maendeleo ya afya zao na jimbo kwa
ujumla.
Alisema
njia mojawapo ya kuwa na afya bora ni kushiriki michezo mbalimbali na hivyo
aliahidi mashindano mengine ya mieleka ambayo yatafanyikia kwenye Kata ya
Mugango mapema mwezi Aprili.
Aliwataka
wananchi hususan vijana kujitokeza kwa wingi na kwamba washindi watapewa zawadi
ambayo alisema ataitangaza siku nyingine.
Aidha,
alisema kila Kata iandae washiriki wawili kwa ajili ya kushiriki mieleka na
wananchi wajiandae kushuhudia mashindano hayo ya kihistoria kuwahi kutokea
Musoma Vijijini.
Mashindano
hayo ya mitumbwi jimboni humo yalishirikisha jumla ya Kata tisa huku kila
mtumbwi ukiwa na washiriki kati ya watano hadi saba na vilevile timu moja ya
kimataifa ya rafiki zake na mbunge huyo kutoka Ujerumani ilishiriki na kushika
nafasi ya mwisho.
No comments:
Post a Comment