Saturday, January 21, 2017

Mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (wa pili kushoto) akifuatana  na Makamo Mkuu wa Chuo Prof. Idriss Ahmada Rai pamoja na Viongozi wengine katika Gwaride la maandamano wakati wa   sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma
 Baadhi ya Wahadhiri na wanataaluma wakiwa katika Gwaride la maandamano wakati wa   sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"
 Baadhi ya wanataaluma wakiwa katika Gwaride la maandamano wakati wa   sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (katikati) akiwapungia mkono wananchi na wanataaluma alipowasili katika viwanja vya kampasi ya Tunguu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA"Mkoa wa Kusini Unguja leo katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho (wa pili kulia) Makamo Mkuu wa Chuo cha  "SUZA"Prof. Idriss Ahmada Rai
Baadhi ya wanataaluma wakisimama wakati mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" alipowasili katika viwanja vya kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja palipofanyika Mahfali ya kumi na mbili ya Chuo hicho leo ,ambapo Wahitimu mbali mbali walitunukiwa Vyeti,Stashahada na Shahada
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                         21.1.2017
MKUU wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa Serikali itahakikisha mikopo inatolewa kwa wanafunzi wanaostahiki na kwa fani iliozipa kipaumbele huku akiwasisitiza wanafunzi kuepuka udanganyifu na kuirejesha mikopo hiyo kwa taratibu zilizopo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo  huko katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),kilichopo Tunguu katika Mahafali ya 12 ya Chuo hicho.

Akitoa nasaha zake Dk. Shein aliwataka wanafunzi kuendelea kuitumia vizuri mikopo inayotolewa na wawe waadilifu, ili huduma hizo muhimu zinazotolewa ziwe endelevu na ziwe na manufaa zaidi kwa maendeleo.

Pia, alisema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa wanaopewa mikopo hiyo wanakidhi viwango vilivyowekwa  na kutumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa sekta ya umma wanaotaka kusoma kuziomba taasisi zao kuwasomesha na si Bodi ya Mikopo ya Zanzibar kwani  huo ndio uamuzi wa Serikali.

“Nililazimika kuingilia kati na kusimamisha kwa muda utoaji wa mikopo ili Serikali iweze kujiridhisha na utaratibu uliopo ambao baadhi ya wananchi wakiulalamikia”,alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein kwa mara nyengine tena aliuhimiza uongozi wa Chuo Kikuu cha SUZA kuongeza juhudi katika kufanya tafiti zinazolenga katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbali mbali zilizopo.

Aliitaka SUZA kuendelea kushirikiana na kushauriana na Taasisi ya “COSTECH” na Tume ya Mipango katika masuala mbali mbali yanayohusu tafiti, matumizi mazuri ya matokeo ya tafiti hizo pamoja na suala zima la kutafuta ufadhili kwa ajili ya kufanya tafiti.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wataalamu Wazalendo walioitikia wito wake na kutekeleza kwa vitendo kuendesha mafunzo  ya PhD ya Kiswahili na kueleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba itaendeleza juhudi za kuwashirikisha Wanadispora katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika sekta zote za kiuchumi na kijamii.

Alisema kuwa juhudi za Serikali katika kuimarisha kilimo nchini zinakwenda sambamba na kuimarisha sekta ya uvuvi hivyo, Serikali ina lengo la kuanzisha taasisi inayofundisha mafunzo ya uvuvi na taaluma ya bahari sambamba na Kampuni ya uvuvi, uvuvi wa bahari kuu na viwanda vya samaki.

Pia, Dk. Shein alisema kuwa Serikali inafanya jitihada ya kuwa na chuo kitakachotoa mafunzo ya unahodha wa vyombo vya baharini pamoja na mafunzo ya ubaharia, kazi ambayo inapendwa sana na vijana hapa nchini.

Alisema kuwa agizo la Serikali la kuiunganisha SUZA na taasisi tatu za Elimu ya Juu hapa Zanzibar lina umuhimu mkubwa katika kuimarisha utoaji wa mafunzo na kuongeza fursa  kwa wahitimu wa taasisi zilizounganishwa kwa kupata vyeti kutoka Chuo kinachotambulika zaidi duniani.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja kwa Televisheni ya SUZA kushirikiana na ZBC Televisheni pamoja na Kituo cha Kwarara  alichokizindua hivi karibuni na kubadilishana uzoefu na utaalamu ili wafikie malengo waliyoyakusudia. Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutunuku zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo hiho cha (SUZA), Profesa Idrisa Rai, alisema kuwa wahitimu wa mwaka wa masomo 2015/2016 katika ngazi mbali mbali za masomo ambapo wanafunzi 861 wamehitimu mwaka huu kwenye masomo 23 ikiwa ni ongezeko la wahitimu 170 na ongezeko la masomo 8.

Alisema kuwa kati ya wahitimu wa mwaka huu, 62 ni wahitimu kwa ngazi ya Cheti, 440 ngazi ya Stashahada, 356 ngazi ya Shahada ambapo wahitimu 2 walitunukiwa Shahada za Uzamili za Sayansi za  Mazingira na Shahada ya Sayansi ya Kemia.

Pia, alisema kuwa kwa mara ya kwanza chuo hicho kina mhitimu mmoja wa Shahada ya Uzamivu ambae amemaliza masomo yake mwaka huu, ambayo hiyo ni Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili ambayo alitunukiwa na Dk. Shein hii leo.

Aidha, Profesa Rai aliwataka wahitimu hao wasidumazwe na changamoto za ajira na wasikate tamaa, wasichoke kusoma na kujisomea zaidi katika fani  ambazo wana hamu ya kuzifanyia kazi.

Profesa Rai alitoa pongezi kwa wanafunzi wa kike na kusema kuwa mwaka huu wahitimu wanawake wamefanikiwa vizuri zaidi kuliko wahitimu wa kiume, licha ya kuwa na wanafunzi wengi ni wa kike chuoni hapo na matokeo yameonesha kuwa wanafunzi wa kike ni mahiri zaidi kuliko wanaume.

Alisema, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Italia, wataanzisha masomo ya lugha ya Kitaliana somo ambalo litaifanya SUZA kusomesha lugha 8 za kigeni.

Pia, kwa kushirikiana na UNICEF wanatarajia kuanza masomo ya Elimu ya Awali katika ngazi ya Shahada na kuanzisha masomo mapya ya Shahada ya Uuguzi na Shahada za Uzamivu za Elimu na ile ya Usimamizi wa Maliasili na Tabianchi ambapo pia, wameanzisha taasisi ya uvuvi na masomo ya bahari.

Aliongeza kuwa ujenzi wa ukumbi maalum wa Chuo kwa ajili ya Mahafali unaoendelea vizuri na wanatarajia Mahafali yajayo kufayika katika ukumbi huo huku akieleza kuwa mwaka ujao wataanza ujenzi wa jengo kwa ajili ya Skuli ya Elimu hapo Tunguu na jengo kwa ajili ya skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni huko Nkrumah kwa ufadhili wa Serikali ya China.  
 
Akisoma risala kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee alieleza mafanikio yaliopatikana chuoni hapo na kuiomba  Serikali kuwa karibu na Chuo hicho hasa katika fani mpya inazoanzishwa.

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma alieleza mashirikiano yaliopo kati ya Wizara yake na Chuo hicho na kupongeza mafanikio yaliopatikana. 
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
 Wahitimu wa Shahada ya Sayansi na Elimu  walipotunukiwa shada yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
 Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira walipotunukiwa shada yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
 Baadhi ya Wahadhiri wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa na Kikundi  cha Brass Band cha Polisi katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya Chuo Kikuu cha Tifa cha Zanzibar SUZA  yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar "SUZA" (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa   katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Ikulu.

No comments: