Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce
Msiru akizungumza wakati wa ukaribisho wa Madiwani wa Halmashauri ya
manispaa ya Moshi walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo.
Baadhi
ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia maelezo ya
awali ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira
mjini Moshi (MUWSA) alipokuwa akitoa neno la ukaribisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akizungumza wakati wa utamburisho wa Madiwani waliotembelea ofisi za MUWSA.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi aliyeongozana na
Madiwani wa Halmashauri hiyo akizungumza wakati wa ziara ya madiwani
katika ofisi za MUWSA.
Mkuu
wa kitengo cha Mipango na Huduma za Biashara Mamlaka ya maji safi na
usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Tumaini Marandu akitoa taarifa ya
Mamlaka hiyo kwa Madiwani waliofanya ziara katika ofsi za MUWSA.
Diwani
wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akichangia jambo mara baada ya
kusikiliza taarifa ya Mamlaka hiyo katika utoaji wa huduma ya maji safi
na maji taka kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Mkurugenzi ,Joyce Msiru akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa na madiwani katika kikao hicho.
Mkaguzi wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Benson Maro akizungumza katika kikao hicho.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce
Msiru akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Moshi,Michael Mwandezi.(kushoto).
Madiwani wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri walipofanya ziara kutembelea vyanzo hicho na kupata maelezo.
Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo ,Patrick Kibasa namna maji yanavyotibiwa.
Meneja Ufundi wa MUWSA,Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa madiwani mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Njoro ya Goha.
Madiwani
wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya maji safi na
usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuhitimisha ziara
ya kutembea ofisi hizo pamoja na vyanzo vya maji.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment