Na MatukiodaimaBlog
WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga kuanza kugawa bure miche ya zao la Pareto.
Akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao La Pareto mwakilishi wa kiwanda cha PCT Bw. Godfrey Mbeyela jana wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bomalang'ombe na Idete , alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata mbegu.
Alisema pamoja na kugawa bure kwa wananchi waliotayari kulima zao hilo la biashara pia kwa wale watakaojiunga vikundi watapewa ajira ya kuotesha miche ya Pareto na kuiuza kwa kampuni ili kuigawa bure kwa wakulima zoezi ambalo litakuwa kwa mwakani.
"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"
Juu ya soko la zao hilo ambalo miaka ya nyuma Wilaya ya Kilolo ilikuwa akiongoza kwa uzalishaji alisema kwa sasa soko ni uhakika kwani kampuni imekuja kwa kasi ya kuwakomboa wakulima na sasa fedha za mazao zitatolewa papo kwa papo shambani baada ya mavuno na hakuna mpango wa kumkopa mkulima.
Pia alisema bei ya zao hilo kwa kilo kwa wananchi wa Kilolo kwa ajili ya kuhamasisha kilo itanunuliwa kati ya Tsh 20,000 hadi Tsh 30,000.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.
Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo hekari moja ya Pareto japo mazao mengine waliyozoea yakiwemo mahindi kwa ajili ya Chakula kulima hekari nyingi zaidi.
Mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo alisema kilimo hicho cha Pareto ni fursa kubwa kwa wananchi ambao watachangamkia kuanza kilimo hicho.
Awali wananchi walisema kuwa waliacha kilimo hicho na mashamba ya Pareto kufyeka na kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto ila kwa sasa kwa utaratibu huu mpya wapo tayari kuchangamkia kilimo hicho.
|
No comments:
Post a Comment