Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa
kwanza kulia) akiongoza kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikati ni
Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin
Kamuzora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho kimefanyika
leo tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho
kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Bw. Shomari Omar Shomari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji, Bi. Fatma Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za
Muungano na namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
- Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu
kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu kutoka Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara
baada ya kumalizika kwa kikao kazi.
Pichani ni Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora
(wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoratibu
kikao hicho ikiwa na wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment