Msafara wa wawekezaji wa ubia kati ya Mifuko ya PPF, NSSF na Jeshi la Magereza katika Kiwanda cha Sukari katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro wakikagua eneo la mashamba yatakayolimwa miwa kwa ajili ya kiwanda hicho. Eneo la ekari 12,000 zimetengwa kwa ajili ya kuanza kilimo cha miwa.
Katika kuitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano wa Kujenga Tanzania ya
Viwanda, Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza (Corporation Sole)
limeingia ubia na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF wa kufufua kilichokuwa
kiwanda cha Sukari kilichopo Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro.
Kiwanda cha sukari cha Mbigiri kilisimamisha uzalishaji tangu mwaka 1996 kutokana
na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo. Lakini kutokana na kuwa
eneo zuri kimkakati yaani uwepo wa raslimali ardhi ya kutosha, nguvu kazi ya
baadhi ya wataalam wa zamani wa kiwanda hicho, chanzo cha maji kuwezesha
kuendesha kilimo cha umwagiliaji kumezishawishi taasisi zingine kushirikiana na
Jeshi la Magereza kuwekeza katika eneo hili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kukagua eneo la Uwekezaji, Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa amesema
uwekezaji huu utakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira,
upatikanaji wa sukari ya kutosha nchini lakini pia wakulima wa eneo hilo
watapata soko la uhakika la kuuza miwa katika kiwanda hicho.
Aidha Kaimu Kamishna huyo ametoa wito kwa wananchi kutovamiwa maeneo ya
majeshi kwani mengi yamehifadhiwa kwa shughuli za baadae zenye maslahi
mapana kwa taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio amesema matarajio yao ni kuona
kiwanda kinaanza mapema iwezekanavyo hivyo, ametoa wito kwa wananchi wa
maeneo jirani kuchangamkia fursa ya kulima zao la miwa kwa maana sasa
watakuwa na uhakika wa soko lililo karibu nao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kyaharara amesema
kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 30,000 kwa mwaka na
kitahitaji tani 500,000 za miwa hivyo ni fursa nzuri kwa wananchi wa maeneo
jirani.
“Ni matarajio yetu kuwa kiwanda hiki kitaongeza ajira, kitainua uchumi kwa
wafanyakazi na wanakijiji, tutapata wanachama wengi zaidi lakini pia tutakuwa
tumeongeza uwezo wetu vizuri zaidi wa kuwahudumia wanachama wetu kupitia
uwekezaji huu” Alihitimisha Prof. Kahyarara.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye
miwani) na ujumbe wake wakiwasili Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro jana tarehe
26.01.2017 tayari kwa kukagua eneo la uwekezaji wa Kilimo cha Miwa na
Uzalishaji wa Sukari. Wa kwanza nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Prof.Godius Kahyarara, mshauri mwelekezi katika mradi huo ndugu Seleman
Karanga akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF ndugu William Erio.
Ujumbe wa Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha Mbigiri kati
ya Mifuko ya Jamii ya NSSF, PPF na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la
Magereza (Corporation Sole) wakikagua baadhi ya maeneo ya ndani ya kiwanda
cha zamani cha sukari cha Gereza hilo kilichosimamisha uzalisha zaidi ya miaka
10 iliyopita.
Ujumbe wa Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha Mbigiri kati
ya Mifuko ya Jamii ya NSSF, PPF na Jeshi la Magereza wakipata maelezo kutoka
kwa Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) Angolwise Pilla (wa pili kushoto)
ambaye ni mfanyakazi wa zamani kilichokuwa kiwanda cha sukari cha Gereza
Mbigiri kilicho simamisha uzalisha zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Viongozi waandamizi kutoka Jeshi la Magereza, PPF na NSSF wakipata
maelezo ya namna kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri mkoani Morogoro
kilivyokuwa kikifanya kazi kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa kiwanda hicho
Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) Angolwise Pilla (wa nne kushoto).
Viongonzi hao walitembelea kiwanda hicho jana ikiwa ni hatua za awali za
uwekezaji wa ubia katika uzalishaji wa sukari nchini kati ya Taasisi hizo tatu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili
kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo na namna kiwanda cha zamani cha sukari
cha Gereza Mbigiri mkoani Morogoro kilivyokuwa kikifanya kazi kutoka kwa
mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi wa
Magereza (ASP) Angolwise Pilla (wa pili kuli). Nyuma ya Dr. Malewa ni
Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio na wa tatu ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa NSSF Prof. Godius Kahyarara.
Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha sukari cha
Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro. Kiwanda hicho kilisimamisha uzalishaji tangu
mwaka 1996 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo.
Mifuko ya PPF, NSSF na Jeshi la Magereza wako katika hatua za awali za kuingia
ubia wa kufufua Kiwanda hicho ili kuitikia kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya
Tano inayotilia msisitizo wa ujenzi wa viwanda.
Mkuu wa Gereza la Mbigiri Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP)
Charlez Kimbi (aliyeinua mkono juu) akitoa ufafanuzi wa jambo katika ziara ya
kukagua shamba la hekari 12,000 zilizotayari kwa kilimo cha miwa kwa ajili ya
uzalishaji wa sukari.
Maafisa wa Jeshi la Magereza, PPF na NSSF wakipiga kambi polini ili
kuteta jambo wakati wa ziara ya kukagua shamba linalotarajiwa kulimwa miwa
kwa ajili ya kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri kinachotarajiwa kuendeshwa
kwa ubia wa Taasisi hizo tatu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea eneo la uwekezaji
wa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa sukari mradi utakaoendeshwa kwa ubia kati
ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza (Corporation Sole), Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF katika eneo la Gereza Mbigiri Mkoani
Morogoro, jana tarehe 26. 01. 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Jamii wa PPF ndugu William Erio
akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea eneo la
uwekezaji wa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa sukari mradi utakaoendeshwa
kwa ubia kati ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza (Corporation Sole),
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF katika eneo la Gereza Mbigiri
Mkoani Morogoro, jana tarehe 26. 01. 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Jamii wa NSSF Prof.Godius Kahyarara
akitoa maelezo ya ziada kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea
eneo la uwekezaji wa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa sukari mradi utakao
endeshwa kwa ubia kati ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza
(Corporation Sole), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF katika eneo la
Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro, jana tarehe 26. 01. 2017
(Picha zote na ASP Deodatus Kazinja, PHQ).
2 comments:
Mwanzo mzuri
Mwanzo mzuri
Post a Comment