Tuesday, January 10, 2017

HABARI KUTOKA TELEVISHENI


Waziri wa elimu Prof. Joyce Ndalichako azindua maabara ya somo la hisabati na kusema itawezesha wanafunzi kufurahia na kuona urahisi wa kusoma Hisabati. https://youtu.be/yabAxtJ_wJU

Rais John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo atatembelea wilaya za Bariadi na Maswa. https://youtu.be/tug4j3iIj5g

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Dr. Shein amesema serikali yake imeweka mazingira rafiki ya kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ili kukuza uchumi wa visiwa hivyo. https://youtu.be/vU0HjAMGqWE

Serikali mkoani Mwanza imetaifisha tani 3 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa tayari kusafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria. https://youtu.be/BfnOfG6L5MA

Serikali yaiagiza bodi mpya ya baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC kuhakikisha sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa kwa vitendo na kuletea wnanchi maendeleo. https://youtu.be/4wKmOTJ-_cw

Serikali imedaiwa kupoteza mapato kutoka biashara ya mifugo baada ya wafugaji kupunguza idadi ya mifugo kwa kuhofia kukamatwa; https://youtu.be/ckwQ12h7kGU

Serikali imehimiza ushirikiano kati ya bodi na watendaji wa baraza la taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC ili kuongeza ufanisi; https://youtu.be/Nk4y1FKF8WY

Kimbunga kikali kilichoambatana na upepo kimekikumba kijiji cha Muyegela wilayani Buhigwe mkoani Kigoma na kuharibu makazi ya wananchi; https://youtu.be/AhNaeq9U1_k  

Rais Dkt John Magufuli leo amefanya ziara katika shule ya msingi Chato ambako alisoma awali na kuahidi kuiboresha shule hiyo; https://youtu.be/740k8PpVfaM

Serikali mkoani Mwanza inajipanga kufanya operesheni ya kuwabaini watoto walioachishwa shule kwa sababu zisizokuwa na msingi; https://youtu.be/eM9vuWZYXGA

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi inatarajia kuboresha makazi ya wakimbizi kwa kuwajengea nyumba zenye gharama nafuu; https://youtu.be/oFwIuzCSqJ0

Licha ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi kuongoza ufaulu kwa mwaka wa 3, bado inakumbwa na changamoto za miundombinu ya Elimu; https://youtu.be/WaVY3Xs96ow

Wanafunzi wawili kutoka shule ya sekondari Mtwara wanatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Ireland kujifunza zaidi masuala ya utafiti; https://youtu.be/y04UjaW8x44

Mashabiki na baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga wamejinasibu kuibuka na ushindi katika mchezo wa nusu fainali hapo kesho dhidi ya Simba; https://youtu.be/XPmHEzZxcjg

Wazazi na walezi nchini wameaswa kujitokeza na kuwapeleka watoto wao kujifunza mchezo wa Kikapu na kupanua wigo wa ajira kwa vijana; https://youtu.be/-mfNRisV1yE

Wakazi wa Vingunguti na maeneo ya jirani wamejitokeza kwa wingi kulisakata dansi katika mapokezi ya mradi wa nyumba bora na za kisasa; https://youtu.be/VDS53m4GYcM

Shirikisho la mpira duniani FIFA siku ya kesho linatarajia kupiga kura ili kuongeza timu zitakazoweza kushiriki kombe la dunia kufikia 48; https://youtu.be/F9NrnGw9HGk

No comments: