Wednesday, January 11, 2017

HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO


SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amewataka wananchi kulima mazao yanayo vumilia ukame ili kuepuka baa la njaa. https://youtu.be/AOHv7FhXHss

SIMU.TV: Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemhukumu kifungo cha miezi sita mbunge wa jimbo la Kilombero Peter Lijuakali kwa kosa la kufanya fujo kwenye kikao. https://youtu.be/hEDWp-O1TZw

SIMU.TV: Wadau wa habari wakiongozwa na baraza la habari hapa nchini MCT wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 kutokana na sheria hiyo kufinya uhuru wa vyombo vya habari. https://youtu.be/3JP804Hgp_o

SIMU.TV: Serikali mkoani Arusha imesema kuwa busara zilihitajika katika kutekeleza agizo la waziri mkuu la kusogeza mashine za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha Eyasi https://youtu.be/abV4gOr2-_U

SIMU.TV: Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI ameuagiza uongozi wa wilaya ya mafia kumpatia sababu za kutokufungwa kwa mashine ya X ray katika hospitali ya wilaya hiyo licha ya mashine hiyo kufika wilayani hapo zaidi ya miezi mitatu. https://youtu.be/HVoCzl40pMs

SIMU.TV: Halmashauri ya jiji la Mwanza imetakiwa kuanisha maeneo rasmi ya maegesho ya magari ili kutatua mgogoro kati ya wenye magari na wakusanya ushuru. https://youtu.be/QzARZuQXSgQ

SIMU.TV: Halmashauri ya jiji la Tanga imetakiwa kuwaelimisha wananchi ili waweze kuweka mipango itakayo wawezesha kunufaika na mradi wa bomba la mafuta. https://youtu.be/-DIRID1lRCM

SIMU.TV: Taasisi isiyo ya kiserikali ya WASAA ina mpango wa kufanya kongamano la wanawake wanaojihusisha na uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kuwaunganisha na masoko. https://youtu.be/obBn0dmpKEM

SIMU.TV: Serikali imeahidi kutekeleza azma yake ya kurekibisha sheria ambazo sii rafiki kwa taasisi binafsi zinazoratibu shughuli za michezo na burudani. https://youtu.be/aabmMotEgeY

SIMU.TV: Michuano ya kuwania kombe la shirikisho hapa nchini inatarajiwa kuendelea kesho kwa timu zinazoshiriki ligi daraja la pili nchini. https://youtu.be/wR7Hf6Ugcok

SIMU.TV: Mashabiki wa klabu ya soka ya Simba wameonesha furaha kubwa na kushindwa kuzuia hisia zao mara baada ya timu yao kuwatandika watani wao wa jadi Yanga na kuwaondosha kwenye michuano ya kombe la mapinduzi. https://youtu.be/0nZtzc0ojyU

SIMU.TV: Mchezaji wa klabu ya Manchester United Morgan Shneiderlin amefanya vipimo katika klabu ya Everton kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo. https://youtu.be/c4BiUgXeNtI

No comments: