Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi
(kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk
Selemani Sewange wakiweka saini makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili
kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka
kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto
waliosimama) ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye, Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, Kaimu Mhariri wa Habari Leo, Nicodemus Ikonko na Mwanasheria wa TSN, Mwadawa Sakware (kulia)
Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi
(kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk
Selemani Sewange wakikabidhiana makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili
kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka
kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,akizungumza kwenye
sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la HabariLeo,iliyofanyika
leo katika uwanja wa Taifa,jijini Dar.Waziri Nape alisema kuwa Gazeti
hilo lililoanza kuchapishwa rasmi Desemba 21, 2006,limekuwa na mchango
mkubwa sana katika juhudi za kuepuka migawanyiko ya kisiasa nchini, na
kuimarisha juhudi za kuendeleza umoja wa kitaifa.
"Na
hili likiwa ni mojawapo ya malengo ya msingi na kusudio la kuanzishwa
kwa Gazeti la HabariLeo na kwa kweli niwapongeze kwa namna mlivyolifanya
kwa kiwango cha juu kabisa,Muda wa miaka 10 sio mdogo kwa uhai wa
gazeti hasa kutokana na ushindani mkubwa na changamoto mbalimbali
zinazoikabili tasnia ya habari hapa nchini na duniani kote.",alisema Waziri Nape.
Mgeni rasmi,Waziri Nape akizindua bahati nasibu ya watoto waliozaliwa desemba 21,2006,anaeshuhudia pichani kulia Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi
Uongozi wa TSN ukimkabidhi zawadi ya Picha Waziri Nape
Muda wa Cheers kwa meza kuu
Chiaazzzzz
Waziri Nape akiwasha mishumaa iliyowekwa kwenye keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo
Waziri Nape pamoja na uongozi wa TSN ,Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah (kulia) kwa pamoja wakikata keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo
Waziri Nape akiongoza meza kuu kukata keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Waziri Nape akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi
Waziri
Nape akionesha umahiri wake wa kupiga gitaa na kuimba ikiwa ni sehemu
ya kuonogesha maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la Habarileo
No comments:
Post a Comment